Nyota ya mtu ni nini

Nyota ya mtu ni nini

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
Somo letu la leo kwenye elimu za sayansi asili ya mwafrika tutajifunza elimu ya unajimu na nyota kwa kiingereza elimu hii inaitwa astrology.

Nyota ni nuru ya mtu ukuu na dira, nyota ni kama kimvuli au aura ya mtu na matumaini yanayoelezea kila kitu kuhusu mtu kuanzia anapozaliwa hadi siku anakufa, nyota imebeba historia ya maisha ya mtu, ni nguvu ya matumaini yaliyofungwa ndani ya mtu katika ulimwengu wa kiroho, kila kitu kuhusu maisha na hatma imefungwa ndani ya nyota yako, mwenye nyota anakua na uwezo wa utofauti na kipaji cha asili kisicho cha kawaida,

Nyota ni nuru na nishati ni kitabu ambacho ndani yake kumeandikwa historia ya maisha ya mtu, kumbuka nyota ya mtu si kama nyota za angani bali nyota ni matamko au maneno yaliyotamkwa juu ya kiumbe na hayo matamko yalipuliziwa uhai na kujifunga pamoja kama kiumbe hai kinacho ishi katika ulimwengu wa roho, ndani ya nyota yako kumeandikwa kila kitu kuhusu wewe na shughuli zote kuanzia kuzaliwa na ndani umefungiwa muda,

Muda ni kama nyakati na majira huu muda kazi yake katika nyota ni kufanya yale matumaini yaliyofungwa katika nyota yako yatokee wakati gani, kila kitu katika maisha kina muda wake wa kutokea, nyota ni kitu uliumbiwa ili kukufanya uwe na hatma ya utukufu uliotukuka, matumaini, matamko na maneno hayo ndani ya nyota yanapofungwa na muda pia hufungwa yaani nyakati na majira, kitu wanachofanya wachawi huzuia ule muda, muda ndio kila kitu, nyota haiibiwi kinachoibiwa au kuchafuliwa ni muda na nyakati ndio maana hapo mwanzo ziliumbwa mbingu na nchi ikisema mwanzo ni huo muda unaojumuisha wakati uliopita, wa sasa na baadae/ujao yaliyobeba matukio, muda ukiibiwa basi tena hakuna nyota, hakuna anaezaliwa na nyota chafu ila watu wabaya ndio huchafua watu wengine, nyota hufungamana na damu, damu ni kiwakilishi cha nyota, ndani ya damu kuna uhai.
Nyota ipo juu ya utosi ambako kuna mwanga wa kiroho ndani ya mwanga kuna muda na ndani ya muda kuna nyota..
 
Nyota ni nuru ya mtu, ukuu na dira- ni kama kivuli au aura ya mtu.
Ndugu mwandishi, Hapa panahitajika ufafanuzi zaidi
 
Tumshukuru mama
IMG-20241007-WA0000.jpg
 
•:-
Somo letu la leo kwenye elimu za sayansi asili ya mwafrika tutajifunza elimu ya unajimu na nyota kwa kiingereza elimu hii inaitwa astrology.
Nyota ni nuru ya mtu ukuu na dira, nyota ni kama kimvuli au aura ya mtu na matumaini yanayoelezea kila kitu kuhusu mtu kuanzia anapozaliwa hadi siku anakufa, nyota imebeba historia ya maisha ya mtu, ni nguvu ya matumaini yaliyofungwa ndani ya mtu katika ulimwengu wa kiroho, kila kitu kuhusu maisha na hatma imefungwa ndani ya nyota yako, mwenye nyota anakua na uwezo wa utofauti na kipaji cha asili kisicho cha kawaida, nyota ni nuru na nishati ni kitabu ambacho ndani yake kumeandikwa historia ya maisha ya mtu, kumbuka nyota ya mtu si kama nyota za angani bali nyota ni matamko au maneno yaliyotamkwa juu ya kiumbe na hayo matamko yalipuliziwa uhai na kujifunga pamoja kama kiumbe hai kinacho ishi katika ulimwengu wa roho, ndani ya nyota yako kumeandikwa kila kitu kuhusu wewe na shughuli zote kuanzia kuzaliwa na ndani umefungiwa muda, muda ni kama nyakati na majira huu muda kazi yake katika nyota ni kufanya yale matumaini yaliyofungwa katika nyota yako yatokee wakati gani, kila kitu katika maisha kina muda wake wa kutokea, nyota ni kitu uliumbiwa ili kukufanya uwe na hatma ya utukufu uliotukuka, matumaini, matamko na maneno hayo ndani ya nyota yanapofungwa na muda pia hufungwa yaani nyakati na majira, kitu wanachofanya wachawi huzuia ule muda, muda ndio kila kitu, nyota haiibiwi kinachoibiwa au kuchafuliwa ni muda na nyakati ndio maana hapo mwanzo ziliumbwa mbingu na nchi ikisema mwanzo ni huo muda unaojumuisha wakati uliopita, wa sasa na baadae/ujao yaliyobeba matukio, muda ukiibiwa basi tena hakuna nyota, hakuna anaezaliwa na nyota chafu ila watu wabaya ndio huchafua watu wengine, nyota hufungamana na damu, damu ni kiwakilishi cha nyota, ndani ya damu kuna uhai.
Nyota ipo juu ya utosi ambako kuna mwanga wa kiroho ndani ya mwanga kuna muda na ndani ya muda kuna nyota..
Nani hua anayasema hayo maneno au matamshi ambayo yanageuka kua nyota ya mtu?
 
Anhaa kwahio ni Mungu sasa ndo hua anagawa hizo nyota wakati mtu anaumbwa
Yes kila
Anhaa kwahio ni Mungu sasa ndo hua anagawa hizo nyota wakati mtu anaumbwa
Mwanadamu anakipawa chake cha jinsi ya kuishi sema elimu za darasani Zinazika vipawa vya watu wengi sana ili kuwafanya wawe watumwa wa mifumo fulani kwa faida ya wachache
 
Je mbona hayo mambo huko Africa tu inakuaje ulaya hakuna masikini hakuna maisha magumu na hakuna mwenye nyota mbaya.

Je hauoni umasikini upo Catalyst na mifumo na sio spiritual realm?
 
Je mbona hayo mambo huko Africa tu inakuaje ulaya hakuna masikini hakuna maisha magumu na hakuna mwenye nyota mbaya.

Je hauoni umasikini upo Catalyst na mifumo na sio spiritual realm?
Hapa umeingia chaka mkuu, umaskini hata ulaya upo. Kama huamini fuatilia makala za waafrika waliojidanganya kua wakienda ulaya mambo yatabadilika cha ajabu ndo wamekua maskini zaidi.
 
Yes kila

Mwanadamu anakipawa chake cha jinsi ya kuishi sema elimu za darasani Zinazika vipawa vya watu wengi sana ili kuwafanya wawe watumwa wa mifumo fulani kwa faida ya wachache
Hii ni kweli kabisa. Mimi mwenyewe nimepitia hii hali. Nikaja kugundua kua kuna vitu vingi niko navyo ambayo vimedumazwa kwa muda mrefu na elimu za darasani
 
Hapa umeingia chaka mkuu, umaskini hata ulaya upo. Kama huamini fuatilia makala za waafrika waliojidanganya kua wakienda ulaya mambo yatabadilika cha ajabu ndo wamekua maskini zaidi.
Sawa Mimi naishi Tanzania sijui chochote but don't be blind hizo mnait Nyota za umasikini na utajiri is waste of time nothing exist.
 
Je mbona hayo mambo huko Africa tu inakuaje ulaya hakuna masikini hakuna maisha magumu na hakuna mwenye nyota mbaya.

Je hauoni umasikini upo Catalyst na mifumo na sio spiritual realm?
Uonyeshwi kila kitu kuhusu ulaya only mambo mazuri
 
Sawa Mimi naishi Tanzania sijui chochote but don't be blind hizo mnait Nyota za umasikini na utajiri is waste of time nothing exist.
Labda hujaelewa vizuri. Kwa maelezo ya ndugu yetu, kasema nyota ni ile talanta au kipawa ambacho ni cha asili unazaliwa nacho. Swala la kua tajiri itategemea na akili yako sasa kutumia hicho kipawa chako kukupa huo utajiri. Haimaanishi kua ukiwa na nyota peke yake basi unakua tajiri automatically
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom