Nyota ya Magufuli inang'ara Alhamis!

Nyota ya Magufuli inang'ara Alhamis!

FICKNARD

Member
Joined
Sep 28, 2010
Posts
8
Reaction score
0
1.Amezaliwa Alhamisi
2.Akachukua fomu ya urais Alhamis
3. Akatangazwa msindi Alhamisi
4. Akaapishwa Alhamis
5. Akatangaza jina la waziri mkuu siku ya Alhamis
6. Akatangaza baraza la mawaziri Alhamisi
TAFAKARI KUNANI ALHAMISI?

Alhamisi inavyoakisi nyota ya Dk. Magufuli

dg.png

Rais Dk. John Magufuli
​

Kama ni suala la kusafiria nyota katika maisha, basi kwa Rais Dk. John Magufuli (pichani), Alhamisi ndiyo ya mafanikio zaidi kwake na amekuwa akiitumia katika matukio mbalimbali makubwa, Nipashe limebaini.

KUZALIWA
Dk. Magufuli ambaye kwa sasa ana miaka 56, alizaliwa Alhamisi Oktoba 29, 1959 Wilaya ya Chato mkoani Geita. Hiyo inamfanya kuwa siku muhimu sana kwake katika maisha.

KUSHINDA URAIS
Alhamisi Oktoba 29, mwaka huu, wakati Dk. Magufuli akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), ilimtangaza rasmi kuwa mshindi wa nafasi ya urais kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

KUAPISHWA URAIS
Alhamisi Novemba 5, mwaka huu, Dk. Magufuli aliapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutangazwa mshindi Oktoba 29, mwaka huu.

UTEUZI MWANASHERIA MKUU
Baada ya kuapishwa Alhamisi Novemba 5, mwaka huu, siku hiyo hiyo alitinga Ikulu kwa mara ya kwanza akiwa Rais na kumteua George Masaju, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na kumuapisha siku iliyofuata.

UTEUZI WA WAZIRI MKUU

Alhamisi Novemba 19, mwaka huu, Dk. Magufuli alipeleka rasmi jina aliloliteua la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, bungeni na siku iliyofuata akamuapisha na kulizindua Bunge.

NAIBU MKURUGENZI TAKUKURU
Alhamisi Desemba 3, mwaka huu, Rais Dk. Magufuli, alimteua Valentino Mlowola, kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Lilian Mashaka, aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

BARAZA LA MAWAZIRI
Jana Alhamisi Desemba 10, mwaka huu, Rais Dk. Magufuli alitangaza rasmi Baraza lake la Mawaziri ikiwa ni siku 42 tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kwa ujumla, matukio hayo yanaifanya siku ya Alhamisi kuzidi kuwa ya kipekee zaidi kwa Rais Dk. Magufuli kwani mbali ya kuonekana kuwa siku yake ya bahati, amekuwa akiitumia kufanya matukio makubwa ya kitaifa.

CHANZO: NIPASHE
 
Just a coincidence. .nalo hili la ku discuss..mwisho wa siku Uta connect connect utatuambia ni siku ya freemason. .
 
Ni maamuzi ya mtu tuu... kuipenda siku furani. km mimi ijumaa naipendaga sana yani tena kupita maelezo. na hiyo siku must nisex
 
Baadaye utasema chakula anakula alhamisi
 
1.Amezaliwa alhamisi
2.Akachukua fomu ya urais Alhamis
3. Akatangazwa msindi alhamisi
4. Akaapishwa Alhamis
5. Akatangaza jina la waziri mkuu siku ya Alhamis
6. Akatangaza baraza la mawaziri alhamisi
TAFAKARI KUNANI ALHAMISI?



Kwani umekuja na wazo hili?
Alahamisi ina nini kihistoria?

Thursday : Jupiter A national survey of North American companies concludes Thursday is the most productive day of the week in business. It's no wonder, as Jupiter has a way of lighting a fire under us and getting us moving. Jupiter is the planet of enterprise and expansion. It's also an extremely optimistic planetary energy that can be felt all through the day on Thursdays when we tune into it. Best tasks for Thursdays include: Socializing, networking, marketing. Working with financial tasks such as the stock market or even checkbook balancing will lead to positive results in the long term when done on Thursdays while ruminating in Jupiter energy. Check out more Jupiter meanings here.


[h=3]Maundy Thursday - What does it mean? - Christian Teaching[/h]Maundy Thursday is a Christian observance in Australia. The day, also known as Holy Thursday, occurs during Holy Week and falls on the Thursday before Good Friday. It commemorates Jesus Christ's last supper and the initiation of the Eucharist, which is observed in many Christian churches.
 
Na ndugu mtoa mada umeileta hii topic ijumaa, kwanini usingesubiri mpaka alhamisi ijayo?
 
Kam vipi watu wote humu hakuna ku-coment hadi ifike Alhamisi ...tumeelewana?
 
Back
Top Bottom