Nyota wa Mbabane atua Yanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyota wa Mbabane atua Yanga

Discussion in 'Sports' started by baraka boki, Jun 7, 2011.

 1. b

  baraka boki Senior Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 181
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Sosthenes Nyoni

  KLABU ya Yanga ipo katika hatua za mwisho kumsajili mshambuaji wa timu ya Mbabane Highlenders ya Swaziland, Mohamed Suleiman kuimarisha zaidi safu yake ya ushambuliaji msimu ujao.

  Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Yanga, Luis Sendeu alisema kuwa tayari mazungumzo ya awali baina yao na mchezaji huyo yamefanyika na kudai kwamba kinachosubiriwa ni kukamilika kwa taratibu zilizosalia.

  Suleiman anakuwa mchezaji wa sita wa kigeni kutangazwa kusajiliwa na Yanga wakiwemo Kenneth Asamoah, Haruna Niyonzima, Tonny Ndolo, Yaw Berko na Davis Mwape.

  Alisema kuwa Suleiman anamudu kucheza nafasi zote ikiwemo ushambuliaji na pamoja na winga hivyo wanaamini atakuwa na msaada mkubwa kwao.

  Naye Suleiman akizungumza gazeti hili Makao Makuu ya Yanga alisema: "Nimemaliza mkataba wangu kule kimsingi nataka kucheza soka nyumbani sasa ingawa naangalia maslahi pia.
   
Loading...