Mzawa_G
JF-Expert Member
- Feb 27, 2014
- 669
- 1,479
Angani kuna makundi makubwa ya nyota ambayo yametapakaa huko anga za mbali kila sehemu ambayo yamefanya hata anga la Dunia yetu lipendeze vizuri sana nyakati za usiku.
Nyota nyingi tunazoweza kuziona katika anga la Dunia yetu pengine zengine zimeshakufa muda mrefu tunafahamu kuwa nyota hupitia katika vipindi 3 vyake ambavyo ni kuzaliwa, kuishi nyakati za ujana na kile kipindi chake cha mwisho ambacho ni kufa kwa nyota na kubalika na kuwa shimbo jeusi (blackhole).
Sasa basi kuna nyota nyingi angani tayari zimeshafika katika hatua hiyo ila bado tunaendelea kuziona zikiwa zinawaka kwa kuwa tu baadhi ya nyota mwangaza wake bado unaendelea kusafiri tu kwa muda mrefu kutokea kwenye chanzo chake mpaka kutufikia sisi na kuendelea mbali zaidi kabisa.
Kuna baadhi ya nyota zipo mbali sana na mwangaza wake usafiri kwa miaka mingi zaidi mamillioni kwa mabillioni ya miaka mpaka kutufikia na kumbuka hapa kila nyota huendelea kusafiri na taswira zake mbalimbali.
Kwa mfano wa harakaharaka mwanga wa jua letu husafiri kwa kiasi cha dakika 8 kutoka katika chanzo chake hadi kufika huku duniani kwetu sasa kama itatokea jua letu likabadili rangi na kuwa rangi ya blue basi itachukua dakika 8 zengine kuweza kuonekana huku Duniani kwetu.
Kuna baadhi ya taswira za nyota ambazo tunazoziona sasa kwa kutumia darubini pengine taswira hizo zilishapita miaka mingi sana na kila siku taswira zinaendelea kubadilika badilika kutokana na vile nyota ilivyokuwa ikibadilisha taswira katika kipindi cha maisha yake.
Mwanga husafiri umbali wa kilomita laki 3 kwa sekunde moja na tunafahamu kuwa umbali baina ya jua na dunia yetu ni kilomita millioni 150 na tunafahamu dakika 1 ina sekunde 60 sindio.
(150,000,000 ÷ 300,000 ÷ 60) utapata jibu sawa na dakika 8.3 ambazo ni sawa na muda ambao mwanga wa letu hutumia kutufikia sisi Duniani.
Mwanga huendelea kusafiri kwa sababu mwangaza husafiri kama mawimbi madogomadogo ambayo yana umeme ndani yake mawimbi hayo uendelea kusafiri milele mpaka pale yatakapoweza kugonga vizuizi vitakavyoweza kubadilisha uelekeo au kupunguza kasi yake hiyo.