Mafanikio ya Mwanadamu huwa yanatokana na nyota yake aliyozaliwa nayo; na nyota inatokana na kizazi chake kama ni cha baraka ama cha laana.
Nyota ya mwanadamu huwa ni kudra ya mwenyezi Mungu kumtunuku Mwanadamu, tangu zama za kale na kale wapo watu ama manabii wakuokuwa na baraka tele - mfano mzuri ni Ibrahimu aliyekuwa na mali nyingi nyingi na ukoo wake umebarikiwa vizazi na vizazi; Suleiman na wengine wengi..
Kama huna nyota njema wewe ama wana ukoo wako mnakuwa ni watu wasio na mafanikio yanaweza kuwa na kielimu, kiafya yaani mnakufa kufa tu hovyo hovyo, na hata kiutafutaji - kila unalolifanya husogei mbele, hela kidogo ukiizipata hata hujui zinaishaje ishaje.
Je unaweza kutengeneza nyota yako ikawa inang'a??
Zipo njia mbilli tu za kutengeneza Nyota yako; Moja ni kwa Maombi, kumwomba Mwenyezi Mungu akupe baraka ili ufanikiwe - hapa unahitaji usafi wa mwili pamoja na matendo yako ili baraka za mwenyezi Mungu ziweze zikushukia, wapo walifanikiwa kupitia njia hii ingawa ni wachache mno.
Mbili ambayo wengi wanafikiri ni nyepesi ni hii ya kuamudu MIUNGU wengine, hii huambatana na masharti (Kafara) ili zoezi liweze kufanikiwa.
Zipo mifano mingi tu ambayo imewakuta watu wengi, kasheshe huwa ni namna zoezi linavyofanyika huwa ni la hatari sana kama wewe ni mwoga basi unaweza kukimbia kwa mganga usiku usiku.
Ngoja nikupe mfano wa dogo mmoja alivyolala makaburini kama alivyokuwa anasimulia yaliyomkuta katika haraka zake za kusaka utajiri.
Dogo (21) maisha yamemgonga akaamua kwenda kwa sangoma, kufika pale kaambiwa atatengenezwa ila sharti la kwanza akubali kulala makaburini usiku wa manane hadi alfajiri. Dogo kapelekwa bwana akaachwa kule mida ya saa saba usiku, aisee ile kukaa tu kwenye kaburi akaanza kuona makaburi yanafunuka mifupa inatoka inaongea na kumsema kwa uchungu kwa nini anafanya hivyo; dogo akakomaa tu ili zoezi likamilike, aliyoyaona mengine hawezi kusimulia kama kweli yapo na yanatokea hapa duniani - Dodo akashinda alfajiri akarudi kwa mganga.
Kufika pale akakuta wameshachemsha maji kwenye pipa yanatokota, akaambiwa avue nguo zote abakie kama ulivyozaliwa kisha atumbukie humo ndani ya pipa akae hadi jioni, ndogo akasita na kuogopa sana akasema kama ni utajiri huu basi wacha nife maskini, akalia na kufikiri sana na kujutia maauzi yake.
Baada ya kama saa moja hivi dogo akapiga moyo konde akaamua basi bwana, kama kufa wacha nife tu - lolote na liwe - wafuasi wa mganga ambao wengi wana umri kama yeye wakawa wanampa moyo asiondoke bali atumbukie lakini bila kumwambia ni nini kitamtokea akiingia kwenye lile pipa linalotokota maji ya moto...
Dogo akatoa nguo zake zote akapanda kwenye kigoda kirefu ili aweze kutumbukia kwa urahisi kwenye pipa humo homo ukiendelea kuchochewa...... Dogo akazama mzima mzima, nini kilimtokea ? tukutane sehemu ya pili ya ushuhua wake wa kusaka utajiri.