Nyongeza ya mishahara 2015

Nyongeza ya mishahara 2015

kashata

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2012
Posts
532
Reaction score
552
Wadau tupeane habari hapa ,salary itaongezeka asilimia ngapi kwa watumishi wa umma?.
 
Ni kati ya 3% kwa kima cha juu na 13.5% kwa kima cha chini.
 
Daah 400,000/= mtihani sana huo mshahara hii serikali hii daah inaniuma sana tunafanya kazi basi tu haki ya mungu
 
Nchi ndio maana watu wanakimbilia siasa ndipo kuna hela laki 4 unapanga nyumba..nauli...chakula...umeme..maji...kweli tutafika
 
Kodi imepunguzwa 2 percent no salary icrement msidanganyane
 
kwa nchi makini na kiongozi makini huwa haongezi mshahara bali hupambana kupunguza mfumuko wa bei, kunakuwa hakuna maana kuongezewa mshahara huku vitu vinapanda bei, chukulia mfano unalipwa 400,000 sasa hivi lakini pesa hiyo inauwezo wa kununua 200kg za sukari kwa sasa, lakini mtu anakuongezea laki na kuwa 500,000 halafu sukari inapanda na kuuzwa 3000 kwa kilo kwa maana hiyo utapata 166 kg na siyo 200 kg tena, na mtu huyo ataenda akijitapa mshahara umepanda bila kujua yeye ndiyo kaibiwa, nchi kama zambia ukipandisha mkate wanaandamana bei ishushwe hawaandamani waongezewe mshahara, watanzania inabidi tuanze tuwe tudai kupunguzwa kwa mfumuko wa bei iwe kwamba kama sasa ninalipwa 400,000 napata kilo 200 za sukari basi niombe serikali ipunguze bei ya sukari kwa kupunguza kodi kukipunguzia kiwanda gharama za uzalishaji ili sukari iuzwe 1500 kwa kilo kwa maana ile 400,000 niliyo kuwa napata kilo 200 sasa nitapata 266 kg kwa maana hiyo laki nne itakidhi mahitaji
 
MR MAJANGA unatumia akili yako vizuri, Mungu akubariki ili akili yako inufaishe jamii.
 
Last edited by a moderator:
Kwa ongezeko tu hili la bei za Petrol, Diesel na Kerosene ni tosha kukujibu kwamba mwaka huu wa 2015 mshahara umepunguzwa badala ya kuongezwa. Hapo sijazungumzia kupanda kwa insurances kwa 18% kazi tunayo wananchi.
 
Tatizo sio mshahara mdogo ila mfumuko wa bei ndio tatizo kubwa kwa wananchi.
 
Itabidi wananchi tuiendeshe nchi badala ya serikali kuiendesha bila manufaa yoyote kwa mwananchi
 
Nchi ndio maana watu wanakimbilia siasa ndipo kuna hela laki 4 unapanga nyumba..nauli...chakula...umeme..maji...kweli tutafika

Unashangaa.. wakati watu wamejenga Gorofa na kununua Vogue na huo mshahara ndani ya miaka mitano...
Hapo ndo uone miujiza ya Musa kuvuka juu ya Bahari..
 
Back
Top Bottom