Nyomi la CHADEMA Arumeru leo

Si mchezo,ila watapiga kura wote?isije ikawa wamekuja kuangalia helkopta
 
Hilo nyomi lote wenye vitambulisho vya kupigia kura hawazidi 50.
 
Kama kweli safi, lakini nakuwa na mashaka maana hiyo picha iko kimya sana, haina maelezo yeyote!!
 
Nitashangaa sana hao CCM wakishinda,Wameru watakua watu wa hovyo kulikoni Igunga.Kwani wameru niwasomi na niwaelewa zaidi
 
Kila siku nasema elimu ya uraia kabla ya chaguzi au wakati hakuna uchaguzi ni muhimu sana
Kuwaeleza watu haki zao na umuhimu wa wao kujiandikisha kupiga kura na kuchagua viongozi wao
Asilimia kubwa ya vijana hawana vile vitambulisho vya mpiga kura na hili ni tatizo la kila sehem
wengi hata waliovipoteza bado hawajapata vingine
Tungeviambia vyama vya siasa kuwa wakati hakuna issue yoyote ya uchaguzi waende huko vijijini wakatoe alimu ya uraia kuwaambia wananchi umuhimu wa kupiga kura na kujiandikisha na umuhimu wa kuwachagua watu au viongozi wanaowapenda na watakaoowaletea maendeleo yao na sio bora kiongozi ambaye anaonekana kwenye kampeni tuu akishapata kura ndo ameondoka
 
Ccm tupo hapa kwenye uwanja mpira chuo cha ualimu patandi naona watoto wa shule msingi ya patandi na wananchi wanapita kwa mbali kama upo karibu na eneo tunaomba ukaribie.
 
Si mchezo,ila watapiga kura wote?isije ikawa wamekuja kuangalia helkopta

Hawa jamaa sijui wanamdanganya nani tizama hao watu wa mbele halafu wanaofata unawaona kwa mbali, picha imechanganywa hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…