Naomba nikiri katika viumbe ninavyoviogopa, nyoka anashika nafasi ya kwanza. Unaweza usiamini hata kuandika jina lake imenigharimu sehemu kubwa ya ujasiri wangu - naogopa hata picha yake!
Pamoja na ukweli huo, nimeshuhudia picha ya nyoka ikitumika kama kielelezo katika sekta ya afya na fedha. Kwa mfano nembo ya hospitali ya taifa Muhimbili ina picha ya nyoka aliyejizungusha kwenye fimbo, kwenye noti ya sh 500 pia kuna picha ya nyoka again akiwa amejizungusha kwenye fimbo.
Ikumbukwe kuwa si muda mrefu sana toka picha za wanyama zianze kutumika kwenye noti zetu badala ya picha za viongozi kama ilivyokuwa awali, nyoka alianza kutumika kabla ya mabadiliko haya. Cha kushangaza watu wa maliasili kwenye matangazo yao ya vivutio vyetu sijawahi kuona wakitangaza nyoka kama kivutio kama twiga, tembo, simba nk wanavyotangazwa.
Sasa nimekuwa nikijiuliza nyoka ana uhusiano gani na tiba na fedha kwa taifa letu kiasi cha kutumika kama kielelezo?
Ndugu Annina usiogope sana nyoka mbona mimi ninaishi nae ndani ya nyumba pamoja kama viumbe wengine?Wa kumuogopa ni Mwenyeezi mungu sio Viumbe wake Ebu ona huyu mzungu anaishi na kiumbe gani?
Mwanamke Anayelala Kitanda Kimoja na Simba na Chui Awashangaza Wengi
Ria akiwa na wanyama wake jikoni Sunday, June 28, 2009 8:37 AM
Mwanamke mmoja wa Afrika Kusini anawashangaza watu wengi kwa jinsi anavyolala kitanda kimoja na kukaa nyumba moja na wanyama hatari 11 wakiwemo simba watano, chui wawili na duma wanne. Picha za mwanamke huyo na wanyama wake mwisho wa habari hii. Wakati watu wengi wakiogopa hata kuwasogelea wanyama hao hatari, hali ni tofauti kwa Riana Van Nieuwenhuizen wa nchini Afrika Kusini ambaye yeye hudiriki hata kulala kitanda kimoja na wanyama hao hatari.
Riana mwenye umri wa miaka 46 akiwaongelea wanyama wake hao anaowafuga ndani ya nyumba yake alisema "Nawapenda sana wote".
Riana alianza maisha yake na wanyama hao hatari kwa kumnunua duma mmoja mwaka 2006 baada ya kugundua kwamba wanyama hao ni miongoni mwa wanyama ambao kizazi chao kinaelekea kupotea kukiwa na duma 1000 tu barani afrika.
Riana aliacha kazi yake ya miaka 22 kwenye kitengo cha wizara ya sheria na kufanya kazi kwa muda kwenye zoo ili aweze kumkuza duma wake.
Riana alitimiza ndoto yake ya kuwaokoa duma baada ya muda mfupi kwa kuanzisha mfuko wa hisani wa kutunza kizazi cha duma Afrika aliouita Fiela Funds Cheetah Breeding Project.
Wanyama wake hao wamekuwa wakiranda randa ndani ya nyumba yake kuanzia jikoni mpaka chumbani kitandani.
Pamoja na wanyama hao wakubwa Riana pia anafuga pia mbwa wawili na paka.
"Hufanya kitu chochote kukujulisha kuwa wana njaa, Wakati mwingine huruka ruka kwenye sakafu kukujulisha kuwa wana njaa" alisema Riana.
Riana ameelezea kufurahia maisha yake hadi sasa na wanyama hao ambao wakiwa porini huwa nyama hazikatizi wakaziachia.
GONGA HAPA KWA PICHA ZA MWANAMKE HUYO NA WANYAMA
WAKE picha hao wanyama bonyeza hapa utaona
http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2353126&&Cat=7