Nyoka aingia kaburini azikwa hai na marehemu

Msindima

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,018
33
Na Said Hauni, Kilwa Masoko

BAADHI ya wakazi wa kijiji cha Makangaga wilayani Kilwa mkoa wa Lindi, wamepigwa na butwaa baada ya nyoka mkubwa kuingia ndani ya kaburi lililokuwa na mwili wa marehemu Mwanawetu Makokola na hatimaye kujilaza karibu na mwili wake.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema lilitokea Aprili 8, mwaka huu saa 10.00 alasiri na kwamba lilisababisha tafrani na hofu kwa waombolezaji.

Baadhi ya waombolezaji, walisema nyoka huyo aina ya jangwa, alijitokeza kwenye eneo hilo la makaburi na kujichanganya na waombolezaji kisha aliingia kaburini wakati likiwa na watu wanne waliokuwa wakiulaza vema mwili wa marehemu.

Walieleza kuwa katika hali ya kushangaza nyoka huyo baada ya kujichanganya na watu hao alijilaza pembezoni mwa mwili wa marehemu huyo.

'' Nyoka huyo aina ya jangwa, alijitokeza kwenye eneo hilo na kisha kujichanganya na waombolezaji na kuingia kaburini ambapo pia alijichanganya na watu waliokwemo ndani ya kaburi hilo kuulaza mwili wa marehemu huyo,'' alisema mmoja wa mashuhuda.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo ni Mwalimu Hamadi Said, Mohamedi Kindamba na Selemani Tengeneza wote wa eneo hilo ambao walisema, baada ya nyoka huyo mwenye urefu usiopungua futi tano na nusu alijilaza pembezoni mwa shimo dogo (mwana wa ndani) ulimokuwa umelazwa mwili huo na kutulia.

Walisema kufuatia kitendo hicho, watu wanne waliokuwemo ndani ya kaburi hilo walitoka nje ya kaburi wakiwa na haja ya kutafuta njia mbadala ya kuweza kumuondoa nyoka huyo ili taratibu za mazishi ziweze kuendelea.

Mashuhuda hao, walisema baada ya mjadala mrefu kupita, ndugu wa marehemu na waliokuwepo kwenye mazishi waliamua kufukia udongo mwili huo pamoja na nyoka bila kumuua wala kumuondoa kutoka ndani ya kaburi hilo.

“Kitendo cha Nyoka huyo kujiingiza ndani ya kaburi, na kuamua kujilaza pembezoni mwa mwili wa marehemu,tulitawanyika kwa muda na kufakari njia tutakayoitumia kumuondoa ndani ya lile kaburi ili tuendelee na taratibu za mazishi ya mwenzetu, lakini zilishindikana,” alisema mmoja wa mashuhuda hao.

Hata hivyo,kutokana na kitendo hicho walichodai ni cha kwanza kutokea katika kijiji hicho, walijiuliza maswali mengi bila kupata majibu yalijitokeza huku baadhi ya watu wakidai tukio hilo linahusiana na ushirikina. Maelezo kutoka kwa baadhi ya ndugu wa marehemu huyo, zinaonyesha kuwa Mwanawetu alifariki baada ya kuugua homa ya malaria kwa muda mfupi, ambapo alifariki saa 4:30 usiku wa Aprili 7, alizikwa Aprili 8, 2009. Hakuna mtu aliyejeruhiwa na nyoka huyo.
 
Kazi ipo utasikia yoote hapo kuwa alikuwa anamfuga ..alikuwa anamtumaa....sasa sijui nini ameamua nae afe nae....nani atamtunza??utasikia yote hayo.
 
Hi story ni kama ya kuuza gazeti! Nyoka ajichanganye na watu, asiwadhuru, wasimuuwe, na akubalizikwe hai.
 
Hi story ni kama ya kuuza gazeti! Nyoka ajichanganye na watu, asiwadhuru, wasimuuwe, na akubalizikwe hai.

Yaani si tu ya kuuza magazeti,pia inatatanisha,nabaki najiuliza ni kweli mambo hayo yanaweza tokea?
 
Back
Top Bottom