Nyimbo za Injili: Changamoto, Vikwazo na Maendeleo

vCTRMA

JF-Expert Member
Jan 12, 2016
306
225
Kwa wapenzi wa Muziki wa Injili Tanzania

Muziki wa Injili hapa kwetu ulianza miaka ya 1980"s kwa kuwa na vikundi vya kwa kwaya na waimbaji binafsi wakiwa na lengo la kuhubiri kwa njia ya muziki (full evangelical muziki).

Uimbaji ulianza kukiwa na aina pekee ya muziki kwa kutumia vyombo vya muziki vya asili na kupelekea muziki huo kuwa wa hali ya chini(local muziki).1990"s muziki wa injili wa Tanzania uliendelea kukua na kuzidi kupendwa ndani na nje ya Tanzania baada ya kuongezeka wasanii wenye vipaji tofauti tofauti na kupelekea muziki huo wa injili kupanuka zaidi..Epharaem Mwansasu, Faustini Munishi, Mzungu Four, Ency Mwalukasa, Cosmas Chidumule , Jenifer Mgendi, Charles Jangalason

Kwaya Ya Lulu, Bara Bara Ya 13 nk walichangia sana mabadiliko katika maendeleo ya kupiga hatua.Nakupekea baadae waje kuzaliwa wasanii maarufu Afrika mashariki na kati wakitokea Tanzania,..kama David Robert kati ya 2002 baada ya kutoa albamu iitwayo BABA.alishirikiana na Godwin Gondwe,..2003 akatoa tena Kijanjani pa MUNGU...ambayo ilipendwa na kupelea D.robert kuwa msanii maarufu wa injili..

2005 na kuendelea wakaja wasanii wengine na kujitahidi kuimba muziki huo wa injili kama Rose Muhando, Christina Shusho, Boni Mwaitege, Jane Misso, Victor Ahron,, Upendo Kilahilo, Catherine Kyambiki, Sara Mvungi, Flora Mbasha, Pst. Abiudi Misholi, Ambwene Mwasongwe, Upendo Nkone, Christina Mwangonda, Jesca Honore, Martha Mwaipaja, Bahati Bukuku na wengineo.

Tangu kuanzia miaka ya 2005.muziki wa injili umekuwa ukishuka sana na kutokupendwa na wadau wengi sana nchini na nje nchi pia..watu wamekuwa wakisikiliza sana muziki wa injili wa nje ya Mipaka kama south afrika kundi ya Joyous cerebration,,nyimbo za tamasha la spirit of praise la south afrika ,zaza,vicky villakazy,n.k....

Naijeria pia akina sinachi na hata afrika ya magharibi,.na kuufatilia zaidi kuliko muziki wa kinyumbani Tanzania..na kupelekea wasanii wa nyumbani kulalama sana kuwa muziki wetu hauna soko ndani ya nchi na hata nje ya nchi na kukata tamaa, wasanii hufanya muziki huo kwa gharama kubwa na kupata hasara sana kwa walivyowekeza pesa nyingi na kupata hasara na hii inazidi kuwa chachu kwasababu wasanii wenye vipawa wanazidi kuogopa na kuzidi kuachana na gospel na kuangalia mambo mengine ya kimaisha ili kuendesha maisha..na kupelekea muziki wa kidunia kushika kasi na kasi zaidi na kuchota wapendwa huku muziki wa injili umekuwa ukishuka...

na hii inachochea kujitokeza watu ambao hawana vipaji na karam za uimbaji kujitokeza na kuimba vitu vya ajabu vinavyofanana na nyimbo za wamataifa na kuzidi kushusha muziki wa injili. kupoteza dhana ya awali ya kuhubiri kwa njia ya muziki,

Na hata wasanii wengine kuiga nyimbo za nje direct au indirect,....sasa ni nini kimechangia hasa mziki wetu kushuka kwa kasi na hadi leo kukosa wapenzi wa muziki huo.?

Mimi maoni yangu kilichochangia kuuwa muziki wetu ni vitu hivi;

1. Ufinyu wa vyombo vya kisasa vya muziki kuendana na soko la muziki-muziki huwaa unaendana sana na teckonolojia,kwahiyo wasanii wetu wanakosa vyombo ili kuzalisha muziki mzuri ambao hata mtu utausikiliza na kupenda mwenendo wa vyombo

2. Kukosa elimu ya muziki-kupata ideas za muziki ni kitu kizuri inasaida kumpa msanii kujua undani wa muziki na kuelewa anafanya nini,wapi ajirekebishe,ajue kuflow,azingatie rhymes.,ajue vocal, nk.elimu ya muziki inasaidia msanii kuwa na ujuzi mzuri na kufanya vitu vya muziki kisomi zaidi ya kawaida ya mazoea..ukiangalia wenzetu wasouth afrika wasanii ukiangalia historia zao huwez kuwa msanii kama huijui fani yako,kujua kutumia vyombo vyote vya muziki kama msanii kuna masharti ya kutafuta melodies,ujue pitch znakuaje nk....ok unaweza ukawa na kipawa cha muziki ila wa kukipalilia na kuchochea ni wewe msanii mwenyewe

3. Baadhi ya wasanii kufanya michanganyo kati ya mambo ya Mungu na mambo ya kidunia na Mungu kuwaacha wafate akili zao wenyewe..kuna baadhi ya wasanii huwa wanashiriki matamasha ya bia na kwenda kushiriki na kuimba kisa pesa,.hii inashusha hadhi ya huu muziki na kuonekana ni wa kawaida kama wa dunia2 ila umetofautiana dhima..

4. Kukosa wasanii wenye vipawa vya kumtumikia Mungu wengi wapo kimaslahi-kuna baadhi ya wasanii ukisikia2 unajua huyu anafosi ila hajui kuimba na hana talent ndani yake.unakuta msanii anaimba nyimbo kakopi kwa solly mahlangu wa south afrika,.pamoja na kuigilizia bado tu anakosea kuimba anaenda nje ya beats..Pia hapa kuna watu wakiwa maarufu2 basi wanataka kuwa wapige show wapate pesa ila ndani yao hawana vipawa vya uimbaji.....na wengi huimba kama wamaifa hadi kucheza pia yani kama wamaifa.,.inabidi tuwe tofauti na wamataifa,..EFESO 4;17

5. Kufunga na kuomba kuombea kipawa au kipaji chako,..wasanii wengi wakipata mafanikio wanatengana na Mungu kisa umaarufu wa duniani wanasahau walitokea wapi na wamefika wapi na wanaelekea wapi,..Tunajua ya kuwa Mungu ni kiongozi wetu kwa kila jambo wasanii wengi huwa wanaanza vizuri tu na Mungu ila baadae wakipata mafanikio wanaachana na Kumtegemea Mungu na kujiona kuwa wanajua na baadae kushuka na kukosa dira tena..

6. Kukosa umoja kwa wasanii husika-wakati haya yote yakitokea sijawahi kusikia hata siku moja wasanii wameitana na kujadili hii hali na kujitahidi kutafuta jawabu ili kutatua shida iliyopo,.ila huwa nawsikia wakilalama tu hawajui wakimbilie wapi..wawe na umoja watafute majibu kuleta mapinduzi ya huu muziki wa gospel..

7. Njia Za kurekodi ni za kizamani sanaa-kwa tunaofahamu muziki kidogo kuna njia inaitwa remote au remote recording,.hii ni kurecord live kwenye tamasha kukiwa na kelele za waskilaji,.hii njia ya kurecord hutumiwea sana na wasanii maarufu duniani,.sifa ya hii recording ni thrilling..hutumiwa hasa na wasanii wa gospel kuleta utofauti na muziki wa injili wa kidunia..hii njia huwa nzuri sana lakini wasanii wetu ni wachache sana wanaotumia hii njia ya recording na ndio hata mimi huwa nawasikiliza japo nyimbo zao bado kidogo ktk utunzi.,..napenda sana kuimba na ni mwanakwaya na najua ntaleta changes 1day na kurudisha uinjilishaji kupitia nyimbo.

Wenzetu huwa wanajifunza kwa makosa na kutumia changamoto wanazo kutana nazo ktk maisha yao ya uijilishaji kupitia nyimbo huboresha na kukuza vitu vyao na hivyo kusaidia muziki wao kupendwa na kukua kila siku na kuzidi kupata soko afrika na duniani kwa ujumla mfano; Sinachi wa nigeria.

Tujifunze kwa wenzetu tusiige tuwe tofauti na tuwe na muziki wetu tupige hatua tuhubiri kwa njia ya uimbaji..watu wanaokoka kupitia nyimbo hizi hizi.
 

mirisho pm

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
3,587
2,000
Tatizo siku hiz hamtofautiani sana na bongo flava... angalia tu hata pics ulizo attach, kumbuka mnamuimbia Mungu,
ni suala la muda tu , watu wataanzakuwachukulia namna mnavyojiweka
badilikeni.
 

kindafu

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,292
2,000
Siku hizi muziki wa Injili umekuwa ni biashara! Kuna wachache wanafanya muziki huu kweli kama Ibada na muziki wao unakuwa na Upako wa kipekee na hubariki wengi katika maisha yao! Ila kuna baadhi wanafanya muziki kwa malengo ya kutengeneza pesa tu! Ukiwaangalia wao wenyewe, tunzi zao, uimbaji na uchezaji wao hakuna uchaji wowote! Ila kwa vile ni soko huria hamna wa kudhibiti!
 

vCTRMA

JF-Expert Member
Jan 12, 2016
306
225
Siku hizi muziki wa Injili umekuwa ni biashara! Kuna wachache wanafanya muziki huu kweli kama Ibada na muziki wao unakuwa na Upako wa kipekee na hubariki wengi katika maisha yao! Ila kuna baadhi wanafanya muziki kwa malengo ya kutengeneza pesa tu! Ukiwaangalia wao wenyewe, tunzi zao, uimbaji na uchezaji wao hakuna uchaji wowote! Ila kwa vile ni soko huria hamna wa kudhibiti!
ni sahii mkuu ni moja ya changamoto.,..watu wapo kifedha zaidi hawapo ktk kumtumikia Mungu zaidi,..
hii nimeianisha ktk kasoro zangu nlizoziwaza zaidi ,..nahii ni njia inayoporomosha injili ya uimbaji....
 

mirisho pm

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
3,587
2,000
mkuu ulitaka wavae nini sasa?????
kanzu?,au wavae magunia mkuu??
Maswali mazuri, ila mtajua wenyewe na biashara yenu ya dini maana mkishashindwa kuimba mnajiita wachungaji....mimi ni muumini wa kawaida tu mkuu...... just know that we are watching you........ pamoja na mapungufu ya kibinadamu lazima mwenendo na tabia zenu na matendo yenu yajitofautishe sana na wasio waamin au wasiomtukuza Mungu katika nyimbo..........Bon Mwaitege alieleza vizur sana.... TAZAMA MATENDO..... ... soon hata waislam wataanza kuimba injili as it will look like it makes no difference... upo ?
 

vCTRMA

JF-Expert Member
Jan 12, 2016
306
225
Maswali mazuri, ila mtajua wenyewe na biashara yenu ya dini maana mkishashindwa kuimba mnajiita wachungaji....mimi ni muumini wa kawaida tu mkuu...... just know that we are watching you........ pamoja na mapungufu ya kibinadamu lazima mwenendo na tabia zenu na matendo yenu yajitofautishe sana na wasio waamin au wasiomtukuza Mungu katika nyimbo..........Bon Mwaitege alieleza vizur sana.... TAZAMA MATENDO..... ... soon hata waislam wataanza kuimba injili as it will look like it makes no difference... upo ?
nimekuelewa mkuu uliyosema nahisi umesoma vizuri post yangu..,..uliyosema ni sahihi na nimesema hapo juu kuwa inabidi tuwe tofauti na wanamusiki wa dunia ili kuleta utofauti kati ya wanamusiki wa injili na wanamusiki wa kumsifu Mungu..
kwa matendo na kila kitu/..
 

Director D

Senior Member
Feb 24, 2016
192
250
Wanamuziki wengi wa injili siku hizi wamekuwa wafanya biashara hili ni moja ya tatizo kubwa kwa sasa,
 

vCTRMA

JF-Expert Member
Jan 12, 2016
306
225
Mkuu Mimi binafsi napendelea kwaya na kwenye kwaya nahisi kasi ya kuchuja ni ndogo tofaut na hao solo artist mfano mzuri tafuta video za my kizito makuburi na mt xavery chang'ombe au my Nauru's kurasini
yah sahihi mkuu...wako vzuri
 

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
4,222
2,000
Hawakawii kusema kuwa kazi za nje zinawaharibia soko wakati bongo flava wenzao wali-shine licha ya wacongo kuwa wako juu.
 

Chosen generation

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
4,380
2,000
Tofautisha kati ya Mziki wa INJILI Vs Mziki wa DINI.

Wengi wanaimba mziki wa DINI siku hizi. Mziki wa INJILI una mashairi yanayolenga kuwaokoa watu kutoka kuzimu. Ni INJILI kwa njia ya nyimbo.

Nawakumbuka ULYANKULU, EAGT Singida, KWA MUNGU HAKUNA MZEE - Shinyanga, Makongoro Choir ya wakati ule nk,..

Nilikuwa navutiwa sana, hawa ndo wamenifanya niupende mziki wa Kwaya sana kuliko wa Solo.

Natamani, mtu aturejeshe enzi za hawa!!!
 

vCTRMA

JF-Expert Member
Jan 12, 2016
306
225
Tofautisha kati ya Mziki wa INJILI Vs Mziki wa DINI.

Wengi wanaimba mziki wa DINI siku hizi. Mziki wa INJILI una mashairi yanayolenga kuwaokoa watu kutoka kuzimu. Ni INJILI kwa njia ya nyimbo.

Nawakumbuka ULYANKULU, EAGT Singida, KWA MUNGU HAKUNA MZEE - Shinyanga, Makongoro Choir ya wakati ule nk,..

Nilikuwa navutiwa sana, hawa ndo wamenifanya niupende mziki wa Kwaya sana kuliko wa Solo.

Natamani, mtu aturejeshe enzi za hawa!!!
ni sahihi mkuu.,...Kuna nyimbo moja ya ulyankulu inaitwa hati ya mashitaka mkuu simchezo,...
haitochuja never zile nyimbo,..
unaskilioza unaskia kabisa upako asee,...wako wapi leo waimbaji wa kushusha upako
 

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
13,492
2,000
Tuanzie hapa, tofauti ya muziki wa injili na kwaya ya kanisa ni nini?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom