jamani mnakumbuka enzi za chama kimoja wanafunzi walivyobadili nyimbo za chama na kuziimba vingine. mfano ''chai, chapati, maharage, mchuzi vyajenga nchi'' badala ya ''chama chetu cha mapinduzi chajenga nchi''. wakati naanza shule nilijua ndivyo zinavyoimbwa mpaka baadae sana baada ya maticha kupiga mkwara ndio ziliimbwa kwa usahihi. kweli wanafunzi walikuwa wabunifu. je wewe una mfano wowote?
alisema, alisema; alisema Nyeree alisema, vijana wangu wote msherekee sasa tuanze mchaka , chinja, tupa............
ukipigwa fimbo ya mgongo utafanyaje; ukipigwa fimbo ya mgongo utafanyaje........ ( wimbo wa kipindi cha majira cha radio Tanzania)