Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,741
- 25,681
Mliopo kwenye ndoa
Naomba mlielewe
Wanandoa wengi sana wamekuwa wakijikuta katika wakati mgumu kwa sababu ya kitu hiki kidogo, SIMU!!! Hebu jiulize! “kwanini wewe unamiliki simu yako na ya mwenza wako? kwanini humuamini mwenza wako? kwanini nawe pia hujiamini? Je kama anakupenda kwa dhati anaweza kukudanganya?
Kwanini usimpe nafasi ajitambue kuliko kuwa mlinzi wa simu yake? Unahisi wewe ukijua anawasiliana na nani kutwa nzima ndio utakuwa na furaha maishani au utaongeza matatizo moyoni mwako na katika mahusiano yenu? Maswali hayo machache tujiulize kabla hatujaenda mbali zaidi na kupelekea kuharibu ndoa. Unadhani simu ndio kigezo cha uaminifu kwake!? Katika hali ya kawaida tu ukifatilia na kukagua simu ya mweza wako kila wakati utajikuta badala ya kupata faraja moyoni unajikuta unapata stress ambazo hazina mpango. Unaumiza moyo wako maana utajikuta unagundua vitu vingi vya ajabu au kutengeneza nadharia mbovu zitakazopelekea mahusiano yenu kuanza kuvurugika.
Uaminifu ni kitu kizuri sana katika mahusiano, muonyeshe mwenza wako kuwa unamuamini sana. Usimfatilie kupita kiasi hasa katika simu yake ya mkononi. Mwache awe na uhuru na simu yake, muonyeshe kuwa bila yeye unaweza kuishi maana ukifuatilia sana simu yake, utaumia na atabaini kuwa bila yeye hujiwezi sikio wala ndewe.
Unajua mtu ukimpa uhuru hata yeye anajishtukia na kushangaa inakuwaje, kwa hiyo hata kama anafanya ujinga atajirudi kwa kuona ni kiasi gani anakukosea na wakati wewe umetulia na unampenda kama kawaida.
Mpende kwa dhati, lakini haimaanishi ndio uwe mlinzi wa simu yake ya mkononi, utajiumiza bure na mapenzi wala hutoona raha yake. Tulia, anayekupenda utamjua tu wala hana macho juu, hana mawasiliano yasiyokuwa na maana, anatulia na wewe.
Hayo mambo ya kua mlinzi wa simu ya mwenza wako ulipaswa uyafanye kipindi upo kwenye uchumba wakati wa kumjua mwenzi wako ni mtu wa namna gani saivi unafanya matendo ambayo hayawezi kubadilisha historia saivi wewe ni mke /mme kama unaona ulikosea kuolewa basi ulikurupuka kwenye uchumba hukuuutumia uchumba ipasavyo
Saivi si wakati wa kupigizana kelel kisa simu.. Huo utoto ulikua kwenye uchumba huko saivi ni wa kukimbizana na malengo yenu