Nyie ITV ZOMBOKO muwongo

Mar 29, 2011
55
18
Jamani ITV huyo Zomboko ni muongo sana. Karibu kila kitu anachoongea kwenye hiki kipindi hawavumi lakini wamo anaongea uwongo mtupu. Wimbo Jamaica Farewell ni Tradional song ya Jamaica na Harry Belafonte alikulia huko, hii hadithi kuwa alimkuta mtu anamwimbia mpenzi wake akauomba ni UWONGO. Pia hadithi kuwa sijui Salim nani sijui alikwenda krekodi na akina Natchil Pitchen wakiwa na Eagles ni UWONGO, wakati Fadhili Williama anaurekodi wimbo huu Eagles haikuweko.ACHENI UWONGO jamani dfah inaudhi
 
Maybe, lakini si kila mtu anaesema kitu usichokikubali (hata kama version ndio ya kweli) ni muongo.
 
Mkuu mwenzako ule ndio ulaji wake kusema uongo kuhusu muziki ... mwache bana....
 
Zomboko amba, siku hiz kila mahali, lalamiko la misha, dunia ya leo ni vuta nikuvute.

Umeshakuwa mtu wa makamo, Zomboko Amba eeeh, na mambo ya uongo hayo, jiepusha nayo...

Muulizeni wimbo huu umeimbwa na nani
 
Zomboko ndiye mkweli muongo ni wewe!. Japo ni kweli Fadhili Williams ndiye mtunzi wa wimbo maarufu wa Malaika, hakuwahi kuurekodi rasmi kwenye santuri waliorekodi ni Eagles na hawakumwandika Fadhili kuwa ndie mtunzi hivyo haki zote za kunakili zinakwenda kwao!.
 
Hata kama anadanganya safi tu, Watanzania tunapenda zaidi porojo na Zomboko ni mahiri kwa hilo badly hata mimi namkubali sana Zomboko.

Kumbuka Masoud Masoud, Charles Hillary na Julius Nyaisanga walipata ujiko wa kutosha kwa kuwa mahili katika kuzidadavuwa nyimbo za zamani mpaka unasikia raha.

Nadhani si vibaya na wewe baadaye ujiandae kuja kuongelea enzi hizo za kina R Kelly, Alli Kiba, Sugu na Twanga pepeta, ila wasi wasi wangu huo muda ukifika watu hawatakuwa wanahitaji kuhadisiwa vitu maana hata kuoa itakuwa unatumia Google search na kuangalia Catalog ya mke umtakae na mahali yake.
 
Mkuu mwenzako ule ndio ulaji wake kusema uongo kuhusu muziki ... mwache bana....

Namfahamu Zomboko na mapungufu yake, nina uhakika kwa 99% kuwa hawezi kuwa anajua JF au internet, ila hili la kumuita muongo si sahihi NA NINA UHAKIKA NALO. JAMANI NAMFAHAMU HUYU MTU!
 
Zomboko amba, siku hiz kila mahali, lalamiko la misha, dunia ya leo ni vuta nikuvute.

Umeshakuwa mtu wa makamo, Zomboko Amba eeeh, na mambo ya uongo hayo, jiepusha nayo...

Muulizeni wimbo huu umeimbwa na nani


Maalim Ghulumo huyo akiwa na OSS ama orchestre Safari Sound.
Hawa jamaa walitamba na vibao vyao vingi sana.,.dah
 
Back
Top Bottom