Na mfano kama huu ndio wengi mnakosea sana sana. Yaani una pick up siku moja au mwaka mmoja na unaacha miaka 20.Huwezi kusifia utawala wa Nyerere wakati vitu vidogo vidogo vya matumizi ya binadamu vilikuwa hakuna..
Wakati wa Nyerere watu tulikosa sabauni za kuongea na kufuria, dawa za meno, vyakula vibovu binadamu wanapewa..
Maduka ya ushirika unapangiwa vitu vya kununua unapewa maharage mabovu pamoja na magadi kwa ajili ya kuivisha wakati unayapika..
Unalazimishwa ununue vitu ambavyo utaki, lazima ununue panga, tube za baiskeli, sigara aina mbili Zakuchuja na Zaraha, mkuki, jembe, spoku za baiskeli za Swala..
Watu wanakwenda shule bila viatu, ukitaka radio mpaka ukanunue RTC..
Ukikutwa na dola 50 utajuta ukiweka akiba ndani ya chakula unaitwa muhujumu uchumi...ukitaka kupiga simu mpaka uende posta upange foleni..
Tumekula chakula cha farasi wa Texas, mahindi ya njano..
Watu walikuwa wanatembea nguo zimetoboka kwenye makalio, viraka kila sehemu..
Ngoja kwanza niishie apa kwanza...
Ukiangalia kazi ya mwalimu kwa sabuni, tv na internet utapata shida kweli kumwelewa. Ukiangalia kazi ya mwalimu in terms of vision, execution and long term sustainable projects unaweza kukosa cha kumsumanga hata kwa bahati mbya tu.
Waberoya,
Mkuu sii umeona viongozi wa vyama wanavyoendesha watu wengine vyamani? Unafikiri ni Unyerere au Ndivyo Tulivyo..Wabunge hadi Ma mayor hujiona wao ni wao waheshimiwa! jambo ambalo Nyerere alitukataza kuwa na waheshimiwa lakini wapi... Mtu akikabidhiwa tu Unyapala basi yeye ndio Mungu mtu ilikuwepo toka utumwa na hadi magerezani kwa wafungwa, nyapala hujiona mkubwa kama Mungu.. Ni hulka ya mtu mweusi..
Ukiangalia kazi ya mwalimu kwa sabuni, tv na internet utapata shida kweli kumwelewa. Ukiangalia kazi ya mwalimu in terms of vision, execution and long term sustainable projects unaweza kukosa cha kumsumanga hata kwa bahati mbya tu.
Aaaah hata mimi nimo mkuu wangu napenda Unyapala wala siwezi kukataa lakini tofauti tu ni kwamba najua ni makosa na najitahidi kutokuwa Nyapala kujiona Mungu mtu...Nimekatazwa na vitabu lakini inferiority complex mkuu ni challenge kubwa sana kwa mtu mweusi utumwa umetufundisha mengi matamanio.. Waswahili wanasema - Maskini akipata makalio hulia Mbwataaa ... yaani kapumzika na kasahau alikotoka, Ndivyo Tulivyo...Ila sii vibaya kupeana tahadhali..Hulka ya mtu mweusi ndio nini bana acha kutuchanganya wewe?? nyerere mweusi au mweupu? unasifia mweusi moja unadharau weusi wote ukiwemo wewe?? ipi ni ipi? Tabia haina rangi mkuu
Mkuu wangu Hivi kweli ukicheza mpira na 4-4-2 ukashindwa ina maana mfumo huo haufai hata kama unajua fika kwamba refa hakuwa upande wenu, jamaa walicheza rafu mwanzo hadi mwisho.. Haya tumepata penalty dakika za mwisho mshambuliaji wetu akapiga juu kama walivyofungwa Ghana na Uruguay bado kosa ni la Kocha...halafu leo Suarez ndio kapewa sifa za kudaka mpira golini na kuwa mchezaji mzuri wa ku sign contract kubwa kubwa kumbe racist..Ama kweli kazi tunayo.Uko sahihi kabisa, tunatofautiana ufahamu na hakuna aliyewahi kudadavua hili kwa undani, lengo lake lilikuwa ni nini?, inaonekana kwa wengi ilikuwa ni hadithi au ndoto fulani....bahati mbaya visions za mwalimu zilikuwa zake, alitumia ubabe mwingi kwa kudhani ana akili nyingi na yuko sahihi...same habit ambayo inaonyeshwa na pro-Nyerere wengi humu..ubabe na kuona wengine mazezeta au mambumbumbu! eti kisani visionary kuliko wengine wote..this is very wrong approach, poor leadership! ndio maana kule CCM leo ukiacha hawa wanaojiita watetezi wa mwalimu kwenye mitandao hakuna anaye-exercise tabia na siasa za mwalimu..they have long gone with him...ila eti anabaki visionary! guys strength are measured in the things we stand for, and weakness manifested in the things we have failed! Kinachobaki ni kuwa goli limefungwa tumeshindwa tunabaki kusema unajua tulipiga sana chenga, tukawapiga kanzu na kosa kosa nyingi...halafu formation yetu tuliyoicheza ya 4-4-2 was the best! yet we have failed
Mbaya zaidi waliofuata hawakutaka kujua tumefeli wapi , wakaanza maisha mapya kabisa, tunabaki Arusha declaration , ujamaa na kujitegemea...my foot! AD mababu zetu wali-support kwa nguvu zote! walitembea miles kwa ajili ya hiyo..leo wote hao wamesahau maumivu na uchungu wa maandamano yale! it seems they supoorted something they never believed! inauma!
kuna watu wako tayari kutukana yeyote wakimtetea Marehemu Nyerere.....kisa alikuwa na akili na hakuna moja leo tunaloringia la mwalimu!!!.......Mwalimu alisema EL hafai...Kikwete ambaye likuwa mtoto wa Nyerere akampa uwaziri mkuu!!!! what happened guys??
mimi mwalimu mwanafunzi akifeli sio tu anaangaliwa mwanafunzi bali na mwalimu wake!!
Sio kwamba alijifanya ana akili, ni kweli alaikuwa na akili na uwezo wake unapimwa katika mizani ya kimataifa bila ya yeye kuwepo. Hata wapinzani wake wanakiri ana akili.Waberoya;3022613]alitumia ubabe mwingi kwa kudhani ana akili nyingi na yuko sahihi...same habit ambayo inaonyeshwa na pro-Nyerere wengi humu..ubabe na kuona wengine mazezeta au mambumbumbu! eti kisani visionary kuliko wengine wote..this is very wrong approach, poor leadership!
Ni kweli mwalimu aliondoka na yake na hakuna anayefuata ndiyo maana kuna akian RA,EL, Jairo n.k. Wanaitafuna nchi.Ndio maana kule CCM leo ukiacha hawa wanaojiita watetezi wa mwalimu kwenye mitandao hakuna anaye-exercise tabia na siasa za mwalimu..they have long gone with him...
Formation haina matatizo, tatizo ni kuwa wachezaji walilala makaburini wakigangwa na viongozi wanatafuta mchawi makaburini hata yule aliyefariki wanadhani ndiye sababu, mashabiki hawajui kwanini tumefungwa wanadhani mganga mzuri ni yule wa Tanga kwasababu anavaa kanzu, yule wa kisukuma alikuwa na madogori mengi ndio maana tumefungwa.Halafu formation yetu tuliyoicheza ya 4-4-2 was the best! yet we have failed
Na kuna watu wapo tayari kusema uongo na uzushi kuhusu Nyerere hata kama hakufanya. Wapo wanaodhani angekuwa pagani nchi hii ingekuwa mbali sana.kuna watu wako tayari kutukana yeyote wakimtetea Marehemu Nyerere.....kisa alikuwa na akili na hakuna moja leo tunaloringia la mwalimu!!!.......Mwalimu alisema EL hafai...Kikwete ambaye likuwa mtoto wa Nyerere akampa uwaziri mkuu!!!! what happened guys??