Nyerere na Karume si msahafu

Nyerere na Karume si msahafu

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Hawa ni waasisi wa Muungano wetu wa Srikali mbili ulioundwa rasmi mnamo tarehe 26 Aprili 1964. Ni hawa ambao walichambua mazingira na hoja zilizokuwepo katika Zanzibar na Tanganyika na kuamua walivyoamua. Ni hawa waliotuwakilisha katika kuuunda Muungano huu jinsi ulivyo. Yaani,Muungano wa Serikali mbili. Waasisi hawa wa Tanzania yetu tunawaheshimu,tunawakumbuka na kuwajali daima.


Lakini, hatupaswi kuyachukulia maamuzi na maneno yao kama Msahafu,kwa maana ya kutobadilika. Muundo huu wa Muungano wa Serikali mbili ulitokana na hekima yao,sababu zao,mazingira waliyoyaona kama viongozi wakuu wa mataifa ya Tanganyika na Zanzibar na kadhalika na kadhalika. Waasisi hawa walitumia kila aina ya ujuzi,ufikiri,mantiki na hoja kufikia hapo kwenye Serikali mbili. Sasa hawapo. Mzee Karume alituacha mwaka 1972 wakati Mwalimu Nyerere alituacha mwaka 1999.

Waliotuacha nasi na Muungano waliouweka ulivyo wao,wametuacha na mazingira tofauti. Mazingira ya kiuchumi,kisiasa,kiutamaduni na kijamii kwa ujumla. Mazingira ya kimaendeleo, ushirikiano na nchi nyingine, nchi kusonga mbele na sayansi na teknolojia. Nchi imebadilika. Hoja za kimuungano haziwezi kubaki vile vile. Lazima zibadilike.

Tume ya Jaji Warioba ilipitia kila ainaya nyaraka ya busara ya Waasisi hawa. Ilitumia nyaraka hizo kama msingi wa kupambanisha ya wakati ule na ya sasa. Wananchi wakasikilizwa na kunukuliwa.Mwisho mwishoni, Tume ya Jaji Warioba ikafika tamati ya kuwa na Serikali tatu. Tume iko sahihi kadiri ilivyoyaona na kuyashuhudia mabadiliko,manung'uniko,malalamiko,miiko.matamko na mihemko ya pande zote za Muungano.

Hoja yangu ni kuwa, Mwalimu Nyerere na Mzee Karume walikuwa sahihi kwa muda wao na matumizi yetu kama nchi. Na Tume ya Jaji Warioba iko sahihi kadiri ya wakati huu tulionao. Nasema Mwalimu Nyerere na Mzee Karume si biblia kwa maana ya maneno,matendo,mawazo na maamuzi yao. Yatabaki kukumbukwa na kutumiwa kama msingi lakini hayatabaki kama nyororo ya kufunga fikra na changamoto za kinchi.

Serikali tatu,moja au mbili ni maamuzi yetu.Lakini, Waasisi wasitufunge kubadilika

cc Waberoya Nguruvi3 Yericko Nyerere, Ben Saanane Chris Lukosi Mzee Mwanakijiji Mamndenyi FaizaFoxy MSALANI Simiyu Yetu ifweero Ruttashobolwa Pasco zumbemkuu JokaKuu na wengineo karibuni kwa mjadala
 
Last edited by a moderator:
Hata katika Biblia kuna Agano la kale na Agano jipya. Ya Nyerere na Karume ni mapatano ya kale ambayo kwa sasa yamegubikwa na kero ni kama Agano la kale. Kwa sasa kwa mazingira haya na sababu za sasa lazima kuwe na mapatano mapya au agano jipya.
 
Mzee Waryoba: “Muungano wa Serikali mbili
waliotuachia waasisi siyo uliopo sasa.
Umebadilishwa mara nyingi, wakati
mwingine bila ya kufanya
mabadiliko kwenye Katiba. Waasisi
walituachia Muungano wa nchi moja
yenye Serikali mbili na siyo nchi
mbili zenye Serikali mbili,”
 
Hata katika Biblia kuna Agano la kale na Agano jipya. Ya Nyerere na Karume ni mapatano ya kale ambayo kwa sasa yamegubikwa na kero ni kama Agano la kale. Kwa sasa kwa mazingira haya na sababu za sasa lazima kuwe na mapatano mapya au agano jipya.

kweli kabisa.naona umeacha kumalizia japo wasabato wanaendelea kushikilia yote ya agano la kale lakini ukichukua wakristo wengine waliowengi wamaona baadhi ya mambo yaliyokatazwa agano la kale yameruhusiwa agano jipya
 
Bora hata muungano ambao ccm inaupigania ingekuwa ni ule ulioasisiwa na nyerere na karume - nchi moja. Muungano wa waasisi haupo tena, hivi sasa ni nchi mbili serikali mbili. CCM wasifanye wananchi wajinga.

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.




Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Muungano uliopo hata Nyerere hakuuacha.Huu ni wa kwetu sisi na mwaka huu tutaubadili tutakavyo
 
Hilo uliloandika mleta mada linawasumbua watu kuelewa.
Nyerere aliua mfumo wa vyama vingi. Muda ulipotimia kutokana na kubadilika kwa mazingira ya kiuchumi, kijamii na kisiasa mfumo huo ulirejeshwa, tena Nyerere akitia baraka zake.

Alikwenda Jangwani kumbadi mgombea wa CCM na kuongea kama kiongozi na si mwanasiasa. Nakumbuka alisisitiza watu kujiandikisha na kupiga kura, na kuhoji kama yupo mtu anayependwa kubebwa, mtu huyo amevunja sheria gani ya nchi?

Wakati wa muungano, Karume alimwambia wewe Rais mimi makamu. Na wakati huo hatukuwa na kizazi cha sasa kinachohoji kwanini ABCD. Iweje leo lionekane ni jambo la ajabu sana kutafuta njia inalyolingana na mazingira yetu!

Muungano wa serikali mbili unaosemwa haupo. Zanzoibar imeuvunja mwaka 2010. Hao wanaoutumia ni kwasababu hawana hoja. Kikwete amekuwepo muungano ukivunjwa, leo anaushujaa gani wa kumnukuu Nyerere hata kwa bahati mbaya.
 
Kwanini tulazimishe Muungano? uwe wa Serikali moja, mbili, tatu? Mimi nauliza, huu muungano feki ambao hauishi malalamiko, una faida ipi kwa Tanganyika na au Zanzibar?

Mimi rai yangu uwe wa Serikali mbili huru, na ya tatu iwe Serikali ya muungano, isiyo na executive powers.
 
Sina cha kuchangia tena hoja zangu zote warioba amezimaliza

Tusubiri lakini la mwisho kama CCM watalazimisha 2 bora hii katiba mpya isimalize salama ili ipatikane heshima.
 
Bora hata muungano ambao ccm inaupigania ingekuwa ni ule ulioasisiwa na nyerere na karume - nchi moja. Muungano wa waasisi haupo tena, hivi sasa ni nchi mbili serikali mbili. CCM wasifanye wananchi wajinga.

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Ni kweli kabisa Mkuu.Tanganyika na irudi kwanza
 
Sina cha kuchangia tena hoja zangu zote warioba amezimaliza

Tusubiri lakini la mwisho kama CCM watalazimisha 2 bora hii katiba mpya isimalize salama ili ipatikane heshima.
Tupo pamoja Mkuu katika hili
 
Uliloliandika lina maana sana. Tutakuwa jamii ya ajabu sana kama tutashindwa hata kuangalia mazingira tuliyomo sasa. Nianavyo mimi ni kwamba hili la waasisi wa muungano linatumika kama chambo tu ila sababu hasa za kung'ang'ania hizo serikali mbili wanazijua vizuri hao wahusika.
 
Back
Top Bottom