Oscar Pius Blog
Member
- May 5, 2015
- 34
- 67
`Kuna mambo mawili ya lazima katika demokrasi,ukiyakosa hayo demokrasia hakuna.
La kwanza:
Ni kwamba kila mtu lazima aweze kusema kwa uhuru kabisa na maneno ya kila mtu lazima yasikilizwe.
'hata kama maneno ya mtu huyo hayapendwi kiasi gani,au walio wengi wanamdhania amepotoka kiasi gani si kitu,kama mtu anapendwa kwa wema wake au hapendwi kwa visa vyake hayo yote si kitu.```
```Kila mtanzania,kila mtu kijijini,kila mjumbe wa halmashauri ya wilaya,kila mbunge na kadhalika lazima aweze kusema kwa uhuru bila vitisho!ama katika mkutano au akiwa nje ya mkutano.
Watu wenye mawazo tofauti hata wakiwa wachache lazima wawe na haki ya kutoa mawazo yao katika majadiliano bila ya hofu ya kushambuliwa,mawazo yao lazima yashindwe katika hoja za majadiliano sio kwa vitisho au mabavu.
Majadiliano yenyewe yatakayoleta uamuzi lazima yawape watu nafasi ya kusema kwa uhuru kabisa,hata baada ya kuamua jambo watu wawe na uhuru wa kuendelea kulizungumza jambo hilo.
Maana wale wachache wenye mawazo tofauti lazima wafahamu kuwa wanayo mawazo yenye maana na kama wakiyaeleza mawazo hayo vizuri wanaweza kubadili mawazo ya wengine walio wengi.```
```Kadhalika wale walio wengi wawe tayari kuyashikilia mawazo yao mpka wale wachache waridhike kwamba uamuzi uliofanywa juu ya jambo lile ulikuwa sawa.```
```Majadiliano lazima yaruhusiwe kuendelea kwa uhuru kabisa,hiyo ni sehemu ya maana ya uhuru wa mtu binafsi.```
*J.K.NYERERE*
_Binadamu na maendeleo_ 1974