amakyasya
JF-Expert Member
- Jun 26, 2013
- 3,480
- 918
Wana JF;
Tarehe 14 October ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha Mwl. Julius Nyerere ambapo Taifa zima linatumia siku hiyo kutafakari mchango wake katika harakati za ukombozi wa nchi yetu ya Tanganyika.
Kama muasisi pia wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwl. Nyerere alikiweka chama kikiwa katika hali nzuri ya maadili akikemea kwa nguvu zake zote Rushwa kama adui wa haki nchini. Kwa sasa hivi ndani ya chama kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa maadili tofauti na alivyokiacha mwl, ikiwemo rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa kila namna na pengine wale wote aliowakataa kwenye uongozi kwa ajili ya kashfa kama hizi leo hii wapo kwenye uongozi wa chama na serikali. Si hivyo tu na wengine wapo kwenye harakati za kutaka kugombea urais.
Je, kwa hali ilivyobadilika ndani ya chama kwa sasa tofauti na misimamo mizuri ya kimaadili alioicha Mwl. Nyerere ambapo viongozi wamebaki kunyosheana vidole kwa tuhuma mbalimbali kiasi cha kuweka mpasuko na makundi ndani ya chama, CCM inamuenzi vipi muasisi huyu?