Nyerere alimaanisha nini kusema hivi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere alimaanisha nini kusema hivi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mzambia, Mar 15, 2011.

 1. m

  mzambia JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  ...Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, na imani mliyonayo juu yetu, tunapata,
  na tutazidi kupata nguvu za kuendesha serikali yenu. Lakini tunawaomba
  msisahau, na mara nyingi sana, nimekukumbusheni jambo hili, kwamba
  serikali haiwezi kufanya kila kitu.

  Utajiri wa Tanganyika, bado uko ardhini. Hatuanzi na akiba kubwa ya
  fedha kama Ghana kwa mfano, iliyoanza nayo ilipopata uhuru wake.
  Hatuna mkononi fedha walizonazo ndugu zetu wa Nigeria. Kwa kweli,
  elimu yetu iko nyuma zaidi kuliko Kenya na Uganda.

  Kwa hiyo, tunaanza bila ya kuwa na wananchi wa kutosha, wenye elimu ya
  juu, tunayohitaji katika jitihada zetu za kujenga utajiri wa nchi hii.

  Lakini matatizo haya, hayanitishi mimi, hayawatishi wenzangu, na wala
  hatuombi kwamba yawatisheni ninyi. Tunayaona kwamba ni jaribio tu.
  Lakini jaribio hili, na umasikini, si la serikali tu, ni la kila raia
  wa Tanganyika.

  ...

  HIVI JAMANI ALIMAANISHA NINI HUYU MKUU WA NCHI ALIYETUKUKA?
   
 2. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mwl. JKN aliamini kwmba umasikini utaondoka kwa hatua moja baada ya nyingine. Kwa hiyo ilifikiria kuwekeza kwanza kwenye elimu ili kupata wataalamu watakaoweza kufanyia kazi utajiri uliopo ardhi kwa masilahi ya nchi. Wamekuja mafisadi kwa kisingizio cha umasikini, wameyauza madini yetu yakiwa ardhini ili wajinufaishe wao wenyewe wachache. Lakini mwhisho unakaribia na hatuaangalia huyu ametoka Canada au Caspian. Tutataifisha migodi yote
   
 3. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ..Alikuwa akionesha kuwa Matatizo yalikuwepo, na alikuwa anayajua, huku akiamini pia wananchi na wasaidizi wake pia wanayajua. Pili, alikuwa akionesha NIA YA DHATI, wala si nia ya kifisadi na uroho, kwamba alikuwa amejipanga kupambana nayo-,Tatu, alijipanga kupambana nayo SI KWA PUPA, na uoga wa kufikia hata kuita WATU WAJE WACHIMBE MADINI YETU, nne aliamini kuwa kupambana na matatizo haya ILIKUWA NI MCHAKATO (process)-rejea anaposema 'hatuna watu wenye elimu ya juu wa kutosha, na hili linatupeleka kwenye namba Tano, kwamba alikuwa anamaanisha kupambana na matatizo haya inahitaji KUWEKA VIPAUMBELE..yaani hapa alimaanisha kwa kuwa hatuna wenye elimu ya juu ya kutosha, tusomeshe sasa-ndio kipaumbele..hivyo watu wakasomeshwa (ingawa badala yakuja kuikwamua nchi wengi wamekuwa wezi wakubwa na mafisadi)..Sita, anapowaambia wananchi kuwa 'sisi hayatutishi, na nyie pia yasiwatishe..alimaanisha ilihitaji UJASIRI NA IMANI, DHAMIRA SAFI,katika kujipamba kutatua matatizo hayo..na likuwa jasiri kwelikweli...una mengi waweza kuyapambanua katika maneno ya Mwalimu..hufurahi sana kila ninaposoma na kusikia aliyosema..kila alichosema kilikuwa na maana nyingi zilizotukuka..na ZINAZOHALISIKA(relevant) HADI HIVI LEO...najua kuwa,na naamini na naendelea kusimamia hili kuwa mimi ni mfuasi wa Mwalimu na itaendelea kuwwa hivyo, mpaka pale itakapotangazwa vingine..lakini pamoja na hilo, Mwalimu was real a MAN IN SERVICE FOR HIS PEOPLE....RIP Mwalimu
   
Loading...