kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,686
===
===
Addis Ababa.
===
===
Wakati Umoja wa Afrika (AU) ukitimiza miaka 50 na Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) ukitimiza miaka 10, viongozi kadhaa waasisi barani Afrika wametajwa kuwa mfano wa kuigwa .
Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na aliyekuwa Rais wa awamu ya kwanza nchini Tanzania hayati Julius Kambarage Nyerere.
Hayo yalibainishwa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili unaohusisha wataalamu wa masuala ya utawala bora kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika ulioandaliwa kuadhimisha miaka 10ya APRM.
Wakizungumza katika mkutano huowa siku mbili, unaotumiwa pia kama tafakuri ya utekelezaji wa malengo ya APRM, wachangiaji mbalimbali walieleza kuhusu misingi adhimu ya utawala bora iliyowekwa na waasisi wa Bara hili akiwemo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania.
Akifungua mkutano huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa APRM Afrika, Assefa Shifaa, alimtaja Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chissano
===
===
na Rais wa zamani wa Afrika Kusini,
===
===
Mzee Nelson Mandela kuwa miongoni mwa viongozi walioenzi kivitendo dhana ya utawala bora.
Alisema viongozi hao walienzi dhana hiyo kwa kukubali kuachia madaraka ya urais wakati ambapo wananchi wao wengi bado walikuwa wakitaka waendelee kuongoza.
Mwaka 1964 alipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi mwaka 1984 alipotangaza kungatuka Nyerere na viongozi wengine wawili watatu wa Afrika waliokuja baadaye kama Mandela na Chissano walienzi misingi muhimu ya utawala bora kwa kuondoka madarakani kwa hiari, alisema.
CHANZO: MWANANCHI