Nyati avamia kijiji na kujeruhi watu saba

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,569
9,430
Serengeti. Nyati amevamia Kijiji cha Nyamisingisi wilayani hapa Mkoa wa Mara na kujeruhi watu saba huku watatu kati yao watatu wakiwa katika hali mbaya.

Ofisa Wanyamapori wilayani hapa, John Lendoyan na Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho, Girihuda Gegasa kwa nyakati tofauti walisema tukio hilo lilitokea jana saa moja asubuhi.

Mganga wa Zahanati ya kijiji hicho, Elias Matobera aliwataja majeruhi kuwa ni Julius Kitasho (57), Peter Umeju (37), Flora Juma(6) na Bebina Juma (4).

Wengine ni Emmanuel Bomani, Gomini Mnada na mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina Yopa.

“Kati ya hao, watoto wawili na Peter nimewapa rufaa kwenda hospitali ya wilaya kwa ajili ya huduma zaidi, hao watoto mmoja ameumia kichwani na mwingine tumbo ambalo linazidi kufura,” alisema Dk Matobera.

Akizungumza kwa njia ya simu mmoja wa majeruhi, Kitasho alisema nyati huyo alionekana kijijini kwao saa 12 asubuhi kwenye shamba la mahindi baada ya watoto kwenda kujisaidia ndipo akawajeruhi.

Alisema walipiga kelele ndipo nyati huyo akakimbia. “Wakati anakimbia (nyati) nilikuwa napita kwenye kichaka, ndipo akanichota na pembe zake na kunirusha chini. Baada ya kudondoka alitaka kunikanyaga, mbwa wangu akatokea na kuanza kubweka, hapo aliniacha hivyo nikapata nafasi ya kujiokoa,” alisema.

Mama wa watoto waliojeruhiwa, Neema Miano alisema alikwenda shambani na kuwaacha watoto nyumbani. “Nilishangaa kupewa taarifa kuwa wamejeruhiwa na nyati,” alisema.

Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho, Girihuida Gegasa alisema tukio hilo limesababisha taharuki kijijini hapo kwa sababu halijawahi kutokea.

Ofisa wanyamapori wilaya, John Lendoyani alisema askari wa Pori la Akiba la Ikorongo na Grumeti walikwenda eneo la tukio na kumuua nyati.

mwananchi
 
Mleta mada weka picha ili tuamini, muonekano wa damu ni muhimu sana katika tukio hadimu kama hili. Habari nzuri sana hii, huyu nyati inabidi achukuliwe kishujaa na jamaa wa TANAPA maana anajeruhi ipasavyo.
 
Sasa nyinyi wanaume wa Mara si mnajiona wanaume kuzidi neno lenyewe wanaume.

Ukikutana na Askari Mtu wa Mara huwa wanakuwa na mbwembwe kweli.

Pambaneni na Nyati huyo.......!!!!!

Mkuu hivi nyati unamjua vizuri simba wenyewe huwa wanakuwa wengi lakini huwa hawamwangushi kindezi.
 
Sasa nyinyi wanaume wa Mara si mnajiona wanaume kuzidi neno lenyewe wanaume.

Ukikutana na Askari Mtu wa Mara huwa wanakuwa na mbwembwe kweli.

Pambaneni na Nyati huyo.......!!!!!
Wapambane tu mana hamna namna hapo
 
Mleta mada weka picha ili tuamini, muonekano wa damu ni muhimu sana katika tukio hadimu kama hili. Habari nzuri sana hii, huyu nyati inabidi achukuliwe kishujaa na jamaa wa TANAPA maana anajeruhi ipasavyo.
Sio maneno ya kuongea mtu alie staharabika kwa wakati huu ambao binadamu mwenzio yupo na hali mbaya baada ya kujeruhiwa na huyo nyati.
 
Daah...maisha haya sasa yanazidi kuwa magumu baba j,mjini hali ngumu,ulituambia turudi kijijini kabla ya mwezi wa saba!!nyati wamewahi kavla yetu...baba j tuoneee huruma wenzio tutakimbilia wapi sasaaaa
 
Nyati mmoja ni hatari sana maana kuna sababu zilizomkelekea kuwa solitary kwa hiyo muda mwingi wanakua na hasira kali
 
Back
Top Bottom