NYASA FOUNDATION ni mfuko hewa unaotumiwa kuigandamiza Wilaya ya Nyasa

V2C

Member
Feb 17, 2014
21
2
Imeripotiwa kwamba Mbunge wa Nyasa, Mh.John Komba anakopa hela katika mfuko wa jamii wa LAPF kwaajili ya NYASA FOUNDATION.

Lakini cha ajabu hakuna ofisi ya Nyasa Foundation, viongozi wake hawajulikani. Wanachangisha fedha nyingi halafu maendeleo Nyasa ni duni.

JE WILAYA YA NYASA NI KISIMA CHA MAFISADI NINI?
 
Ni kweli , utafiti unaonyesha kwamba hakuna kabisa kitu kama hicho na hakijawahi kuwepo !
 
hivi huyo komba tumbo lote lile bado anataka kulizidisha kwa kuwizi wa pesa zetu za payee tu jaman.
 
tena afadhari umelileta hapa jf,huu mfuko umeleta migongano mikubwa baina ya wakuu wa idara na viongozi wa kisiasa wilaya ya nyasa,kuna wakati huyu komba alimwalika mh.Lowasa kwenye harambee ya kuchangia huo mfuko,na zilipatikana milion mia mbili ,kitu cha ajabu harambee ilipopita viongozi waliomba hizo fedha kwa ajiri ya kuzifanyia kazi ,lakini cha ajabu komba na rafiki yake mh.mwisho mkiti wa halmashauri wakawapa majibu hizo fedha haziwahusu na wameamua kuwaachia kwa sababu tangu mwaka jana hadi leo hakuna kinachofanyika ,huu mfuko unachangisha ela kwa ajiri ya kufanyia kampeni zao mwakani huu mfuko ni wizi mtupu.Na sasa kawachangisha wananchi elfu ishirini kwa ajiri ya kuwaletea pikipiki ,wizi mtupu,anafanya hayo kwa kuwa anajua hawezi kurudi tena bungeni mwakani ,chukua chako mapema ( ccm) oyeeeeee
 
Wilaya ya nyasa imetekwa na mafisadi na wachumia tumbo, kuanzia mbunge mh. Komba, mwenyekiti wa halmashauri mh. Mwisho, ni wizi kwa kwenda mbele! Kazi ya komba ni kugawa tshirt na kanga tu wakati wa uchaguzi! Amkeni wanyasa wilaya yenu inaliwa..
 
itabidi nifikishe ujumbe kwa mzazi wangu kuhusu hiyo nyasa foundation ili apate elimu na asiendelee kuichangia kama alivyo fanya hapo awali.kumbe ni yale yale.
 
  • Thanks
Reactions: V2C
Back
Top Bottom