Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,249
Nchi ya Nigeria imekumbwa na uhaba mkubwa wa nyanya. Asilimia themanini ya mashamba ya nyanya katika maeneo ya kaskazini inasemekana yameharibiwa na watoto wanaokula kila kitu.Matokeo yake, bei ya bidhaa hiyo imepanda maradufu.
Mji wa Kura, ni mji ambao unajulikana kwa kilimo cha umwagiliaji kilomita thelathini magharibi mwa mji wa Kano uliopo kaskazini mwa Nigeria.
Badala ya majani ya kijani na matunda yake yenye rangi nyekundu, ninachokiona hapa ni majani madogo yaliyokauka. Hii ni ishara tosha kwamba Tuta absoluta, mdodo ambae anakula mizizi, mti, majani na matunda yuko hapa. Mashamba mingi hapa yana muonekano sawa. Shamba la Dahiru Dantsoho ni miongoni mwa yaliyoathirika:
Kura "hii imesababishwa na mdudu tunaemuita sharon ambae anakula mti ikiwemo mizizi, na huacha shamba likiwa limeungua. Tumetumia dawa mbalimbali lakini hazikusaidia, hii imepangwa na Mungu."
Wakulima wanaangalia kwa kukata tamaa jinsi tunda walilolifanyia kazi, likiangamia. Muhammad Idris Kura ni mmoja wa wakulima ambae anasema hata hawezi kuanza kuhesabu hasara walioipata:
Muhammad Idris Kura: anasema "kwa kweli siwezi kukisia hasara niliyoipata, kwa sababu tumefanya baadhi ya kazi hapa sisi wenyewe. Iwapo tutakadiria gharama ya jasho letu, kiwango kitakuwa kikubwa mno, ni kwa sababu hiyo ndio maana hatuhesabu. Kwa mfano hivi sasa, hawa wakulima hawana mbolea ya kutumia mashambani mwao hasa katika msimu wa mvua na hawana chakula pia. Hakuna kitu wanachoweza kufanya zaidi ya kukubali matokeo. "
Image captionNyanya zimeharibika
katika jimbo jirani la Kaduna, serikali imekisia kwamba takriban asilimia themanini ya mashamba ya nyanya yameharibiwa, huku wakulima mia mbili katika jamii tatu wakipata hasara ya zaidi ya dola za kimarekani laki tano.Hata hivyo, serikali ya Nigeria imesema imewapa kazi wataalamu kuliangalia tatizo hilol ambalo limeathiri majimbo sita.
Katika mji wa Kano, hasara hiyo imekilazimu kiwanda cha nyanya ambacho kimeanzishwa na mfanyabiashara maarufu, Aliko Dangote, kufungwa kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo.