Nyanya ni tiba ya kuongeza wingi wa shahawa

QEEN ADEMU1

Senior Member
Dec 24, 2019
134
324
Chakula chenye nyanya nyingi kinaweza kumsaidia mwanaume kutoa mbegu za kiume zenye ubora, utafiti umebainisha. Afya ya wanaume ambao hunywa vijiko viwili vya nyanya ambayo imesagwa kwa siku, wamebainika kuwa na shahawa ambazo ni bora zaidi.

Tatizo la uzazi kwa wanaume limeathiri karibu nusu ya idadi ya wapenzi wanaoishindwa kupata watoto. Mtaalamu wa masuala ya uzazi anasema kuwa kuna uhitaji wa tafiti nyingi zaidi kuhusisha wanaume ili kujua tatizo lao la kushindwa kuzalisha.

Wataalamu wa afya wamewashauri wanaume wenye matatizo ya uzazi kwa sasa kula chakula bora kwa afya na kuvaa nguo za ndani ambazo hazibani.

Utafiti umeshauri pia wanaume wanapaswa kupunguza msongo wa mawazo kadri wawezavyo na kushiriki tendo la ndoa na wenza wao kila mara wanapokuwa karibu na wapenzi wao.

Lakini wazo la kutumia chakula cha aina fulani cha virutubisho limekuwa likisisitizwa sana kwa muda sasa. Nyanya ni chakula ambacho kina vitamini E na madini ya zinc. Jambo ambalo limekuwa likiwekewa mkazo katika tafiti zilizopita ni kuwa na uwezo wa kuzuia seli ambazo zinaweza kusababisha uharibifu katika mwili.

Chakula hicho kimekuwa kikihusishwa na faida za kiafya pamoja na kupunguza hatari za kupata ugonjwa wa moyo au saratani.

Wataalam wanasema kuwa kuna watu wanaotumia tiba lishe kwa sababu kutumia tu nyanya kwenye chakula inawia vigumu kutambua kwa uhakika kama kila mwanaume amepata .

Wanaume wanahitajika kula nyanya kilo mbili zilizopikwa kila siku ili kupata ujazo sawa na tiba lishe ya nyanya.
Katika jaribio la wiki 12, ambapo kampuni inayotengeneza tiba lishe ilichagua wanaume 60 kunywa tiba lishe gramu 14 kwa siku au vidonge. Mbegu zao za kiume zilifanyiwa jaribio la kwanza katika wiki ya sita na mwishoni mwa utafiti.

Licha ya utofauti wa manii zao lakini zilionyesha namna gani shahawa zinatoka kwa kasi ya juu kwa wale waliokula tiba mbadala ya nyanya.

Dr Liz Williams, mtaalamu wa lishe katika Chuo Kikuu cha Sheffield, anasema kuwa sasa kuna ushauri mdogo sana ambao anaweza kuwapa wanaume katika kutumia chakula hicho.

Kuleni nyanya wanaume, huenda ikasaidia kuondoa ukame wa kukosa watoto katika ndoa zenu. Mnaweza kuwa mnawalaumu wake zenu, kumbe tatizo ni shahawa zenu hafifu.

Pia, kumbukeni, msivae nguo za ndani za kubana, zinadhuru kiwanda cha shahawa (korodani). Kule joto halitakiwi kuzidi 35C. Sasa boxer za kubana zitawaponza mkose watoto, mzunguke waganga nchi nzima na bado mkose watoto.
Kinga ni bora.
 
QEEN ADEMU1,
Kilo 2 kwa siku? Ila wazungu wametuharibu sana, mbona humu vijana karibia wote ikitolewa nyuzi ya kugegedana wote wako active katika kula tunda sasa hizo nguvu hazitungishi mimba?
 
Mkuu, hizo nyanya peleka kwa wavulana wa mikoani, wakale ili waweze kuimarisha jinsia zao, siyo kulialia kama MC pilipili iliyochacha
 
Nguvu za kiume nikula balanced diet na kufanya mazoezi tu,hayo mengine ni upuuzi upuuzi tu
 
Back
Top Bottom