Nyani na Sokwe !

Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
3,197
3,930
Katika shule moja mkoani Tanga katika darasa fulani kulitokea mwanafunzi mmoja kuwa mkorofi sana. Yeye katika kila orodha ya wanafunzi watukutu huwa hakosekani. Siku moja baada ya kufanya ukorofi wake alikutana na Mwalimu uso kwa uso na mambo yakawa hivi:
Mwalimu: Wewe nyani njoo hapa
Mwanafunzi: Ndiyo nakuja
Mwalimu: Jina lako nani?
Mwanafunzi: Samahani sana Mwalimu sisi manyani kwetu hatupewi majina sijui nyie masokwe!

Baada ya kujibiwa hivyo tena mbele ya kundi la Wanafunzi, Mwalimu akawa hana hata hamu ya kumuona Mwanafunzi huyo tokea siku hiyo.
 
Back
Top Bottom