Nyani Apandikizwa Moyo wa Nguruwe

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
11.jpg

Moyo wa nguruwe
Maryland, Marekani
WANASAYANSI kutoka Taasisi ya Kitaifa ya Moyo, Mapafu na Damu huko Maryland nchini

Marekani wanasema kuwa wamefanikiwa kuweka moyo wa nguruwe katika nyani kwa zaidi ya miaka miwili.

Matokeo yake yanaweza kupiga hatua katika tiba ya upandikizaji wa viungo vya wanyama katika binaadamu huku kukiwa kuna upungufu wa binadamu wanaotoa viungo vyao.
22.jpg

Nguruwe​

Upandikazi wa viumbe tofauti husababisha mmenyuko wa kinga na kusababisha kukataliwa kwa kiungo hicho na mwili unaofanyiwa upasuaji huo.

Lakini wanasayansi kutoka Marekani na Ujerumani walitumia muundo wa jeni pamoja na dawa zinazopunguza kinga. Kazi yao imeelezea katika jarida la mawasiliano ya kiasilia.
33.jpg

Nyani​

Ni muhimu kwa sababu inaleta uwezekano wa kutumia viungo hivyo kwa binaadamu, kulingana na mwandishi mwenza Muhammad Mohiuddin kutoka Maryland, alikiambia chombo cha habari cha AFP.

Upandikizaji wa kutumia viumbe tofauti unaweza kuokoa maisha ya wengi kila mwaka ambayo hupotezwa kutokana na ukosefu wa viungo vya binaadamu kwa upandikizaji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom