Nyama ya ng'ombe Kwa Watu Wanne | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyama ya ng'ombe Kwa Watu Wanne

Discussion in 'JF Chef' started by Lizzy, Jan 28, 2012.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  LAT recipe hii hapa. . .
  Ntajitahidi niweke picha haraka iwezekanavyo kwasababu zitakuonyesha kila kitu kinavyotakiwa kufanyika na namna gani vionekane which is quite important.

  Mlo wa watu wanne (4)

  Mahitaji
  Nyama ya ng'ombe 1/2 kg
  Cream ya kupikia 1.5 - 2.5 dl /maziwa
  Uyoga kiasi upendacho
  Hoho 1- 3....mimi hua natumia rangi tatu tofauti (Nyekundu, kijani na njano).
  Kitunguu kimoja kikubwa
  Soy sauce kijiko kidogo 1
  Food coloring
  Pilipili manga (black pepper) au white pepper iliyosagwa
  Oregan
  Basil
  Chumvi
  Mafuta ya maji au siagi
  Maji ya kutosha
  Maandalizi

  Katakata nyama yako vipande vidogo vidogo na viungo vingine vyote baada ya kuviosha.

  Andaa frying pan yako na sufuria itakayotosha kuchemsha kila kitu pamoja. Ukimaliza nyunyuzia chumvi na pilipili manga (nusu kijiko cha chai of each) kwenye nyama yako kwa kuisambaza.

  Hatua inayofuata ni kuunguza nyama yako kidogo hivyo weka frying pan na mafuta kidogo jikoni mpaka vitakapopata moto. Vikishapata moto weka nusu ya nyama yako kwenye frying pan na ugeuze haraka haraka. Haitakiwi kutoa maji, inatakiwa iungue tu juu hivyo usije ukaweka kabla mafuta hayajapata moto vizuri. Baada ya dakika 3 weka nyama yako kwenye sufuria uliyoandaa mapema kisha urudishe kikaangio chako jikoni. Chukua maji nusu kikombe uweke kwenye kikaangio kikiwa jikoni iwe kama unakiosha vile. Hayo maji yakianza kuchemka changanya na ile nyama iliyopo kwenye sufuria. Rudia hatua hizo hizo kukaanga ile iliyobakia.

  Ukimaliza kaanga vitunguu, hoho, uyoga "mbalimbali" mpaka vitakapoanza kulainika kisha changanya na nyama.
  Baada ya hapo weka maji vikombe 4-6 vya chai, weka chumvi kidogo, funika na uweke motoni. Acha ichemke kwa dakika 40 - 50 mpaka utakapoona maji yaliyobaki hayazidi theluthi moja (1/3) ya kiasi ulichoweka mwanzo.

  Weka cream (ni nzuri zaidi kwasababu itafanya kitoweo chako kiwe kizito) au maziwa, koroga mpaka itakapoanza kuchemka. Kisha weka kijiko cha chai 1 soy souce na matone. . MATONE matatu tu ya food coloring ya brown/nyeusi, oregan na basil kiasi unachoweza kushika kwa vidole vyako viwili. Onja kujua kama kuna kitu ungependa kuongeza (pilipili manga/chumvi) kabla ya kufunika, kupunguza moto mpaka chini na kuacha cream iive taratibu kwa dakika 6 - 10.

  Unaweza ukala kwa wali, viazi vya kuchemsha pekee bila mafuta au hata pasta za aina yoyote ile.

  PS
  Soy sauce sio lazima ila food coloring ni muhimu ili kuipa mboga rangi ya kuvutia.
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Lizzy, thanks

  i know mushroom inavirutubisho vingi sana ambavyo ni free from colestral and other hazards

  wacha nikaitume na chakula cha uyoga
   
Loading...