Japo labda mapishi huenda yakawa tofauti, kuna wenzetu wanawala kenge vizuli tu.
Miaka ya 2010, tukawatembelea wafilipino huko Mwanza,sasa wao hupika na kubeba sufuria lao mpaka mezani,hakuna cha hotpots. Nyama ukiangalia,haieleweki. Ukiuliza, unaambiwa ula au acha. Tukaona isiwetabu, baada ya kula,kila mmoja anaosha sahani yake jikoni. Dah! Mkia,kichwa na miguu vimeshikana na ngozi viko hapo.
Unawaza kufa,kuugua tumbo au majanga mengine. Masaa,siku,wiki kumbe hakuna kisicholiwa.
Kosa labda kujua unachokula