Mheshimiwa Rais,
Yawezekana hii ikawa sio njia itakayokufikia moja kwa moja lakini naamini viongozi wote huchungulia hapa kila mara ndiyo maana wakati mwingine huilalamikia sana JF.
Mheshimiwa Rais, heshima kwako kwa kuiongoza nchi hii ya Tanzania. Dunia ina nchi nyingi na kila nchi inauongozi wake. tumeshuhudia viongozi wengine wazuri sana kwa maana ya kukubalika na wanachi wake, pia kuonyesha moyo wa utendaji kazi mzuri na kuwasaidia wananchi kwa kiwango kikubwa!
Kuna viongozi wengine wameshindwa kabisa kuwasaidia wanachi wao na kuwaacha wakiwa katika mateso makubwa na hatimaye wameondolewa madarakani eidha kwa fedheha au kwa kunyimwa kura na wanachi wao.
Uongozi ni wito kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wako, tena kwa moyo wa kujitoa yaani ni lazima wewe mwenywe uwe na uchungu juu ya maisha ya wanachi unaowaongoza.
Napenda nianze kupambanua moja kwa moja.
Nyakati.
Tanzania ya sasa inahitaji sana uzisome nyakati hizi. Ukweli ni kwamba wananchi wako wengi wameelimika, teknolojia pia imerahisisha mawasiliano. Leo hii ni rahsi sana kujifunza na kuiga mambo yanayofanyika nchi za mbali kwa vile tu watu wanaona kwenye luninga na kusoma kwenye mitandao. Naomba sana uzitambue nyakati hizi ujaribu kuongoza taifa lako kwa kuendana na nyakati.
Maisha,
Mheshimiwa rais, maisha ni magumu sana kwetu sisi raia wa chini. hivi unafahamu kuwa wengine tunalala njaa? Hebu fikiria tu kwa haraka haraka "sisi juzi tumelala njaa kabisa, kumbe viongizi wengine walilala hotel ya kulipia Tshs 400,000/=?" Hiyo laki nne tungeipata sisi ingetutoa mwaka mzima.
Bidhaa zote zimepanda sana, mafuta, sukari, sabuni, billi za umeme n.k, unakumbuka wakati alikuwepo Mh. Mkapa tulikuwa tunanunua kiberiti kwa Tshs 20? unajua kuwa leo kinakimbilia Tshs 200? Wahurumie wanachi wako mheshimiwa! Panua roho ya kusaidia watu.
Kuwasaidia wanachi wako ni kuwa na mpango madhubuti wa kuhakikisha hata hizi bidhaa zinashuka bei, billi za umeme zinakuwa ndogo. Kwakweli ukifika huku kwetu inasikitisha sana.
Migogoro.
Yaani jana nilifikiria sana nikawaza sana, nikafikia hadi kusema kumbe hata mimi naweza kuwa rais na nikalifanya taifa langu kuwa la amani. Mheshimiwa rais, wewe unajisikiaje migogoro inapokuwa mingi nchini mwako?
Vyuo Vikuu
Madaktari
Walimu
Tatizo la Umeme
Mauaji ya raia yanayofanywa na polisi,
Manesi nao wanalalamika,
Maisha magumu n.k
Haya yote na mengine mengi yanaisumbua sana hii nchi. Juzi wilaya ya rungwe kulikuwa na maandamano walimu wanambana mkurugenzi wa halmashauri awalipe mishahara yao palikuwa hapatoshi ungekuwepo ungeona kweli kuwa hii nchi inahitaji mtazamo mpya katika uongozi.
Mheshimiwa Rais, uongozi wako wote kuanzia ngazi za juu (wizara) hadi huku chini kwa kitongozi wa mtaa huduma zake ni mbaya mno. hivi unafahamu kuwa hizi halimashauri zako za Wilaya zimejaa uozo? Unafahamu kuwa sisi wananchi bila kutoa chochote hatuwezi kuhudumiwa? Tukisema tukaripoti Takukuru tunageukwa na kuonekana wabaya ikiwezekana kukosa huduma kabisa?
Mwananchi anafuatilia leseni ya biashara ili ajitafutie chakula cha kila siku pia alipe kodi TRA kwa faida ya nchi yake, lakini unakuta huyu mtu anazungushwa hadi anakata tamaa je Serikali si imekosa mapato ya bure? Wataalamu wengi husema njia huharibiwa na kiongozi! Rais kama ungekuwa serious na kazi yako hata huku kijijini viongozi wangefanya kazi kwa utii. fikiria haya......
Mwisho,
Mheshimiwa napenda sana kukuomba utumie moyo wa huruma, kama huna mzigo au wito wa kuiongoza nchi ni bora ukawapatia wengine ili kunusuru maisha ya watanzania wengi na hata wewe utoke kwa amani. Tunakokwenda ni pabaya mno, kama wataalamu wameanza migomo unadhani utaenda kujificha wapi? vumilivu umeisha kwa Watanzania wengi nakuomba rais wangu yafikirie haya.
HAKUNA KIONGOZI YEYOTE ANAYEWEZA KUFANYA VIZURI ASIPOKUWA NA HOFU YA MUNGU.
Asante.