Nyakati: Barua ya Wazi kwa Rais wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyakati: Barua ya Wazi kwa Rais wa Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Radio Producer, Mar 10, 2012.

 1. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Mheshimiwa Rais,

  Yawezekana hii ikawa sio njia itakayokufikia moja kwa moja lakini naamini viongozi wote huchungulia hapa kila mara ndiyo maana wakati mwingine huilalamikia sana JF.

  Mheshimiwa Rais, heshima kwako kwa kuiongoza nchi hii ya Tanzania. Dunia ina nchi nyingi na kila nchi inauongozi wake. tumeshuhudia viongozi wengine wazuri sana kwa maana ya kukubalika na wanachi wake, pia kuonyesha moyo wa utendaji kazi mzuri na kuwasaidia wananchi kwa kiwango kikubwa!

  Kuna viongozi wengine wameshindwa kabisa kuwasaidia wanachi wao na kuwaacha wakiwa katika mateso makubwa na hatimaye wameondolewa madarakani eidha kwa fedheha au kwa kunyimwa kura na wanachi wao.

  Uongozi ni wito kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wako, tena kwa moyo wa kujitoa yaani ni lazima wewe mwenywe uwe na uchungu juu ya maisha ya wanachi unaowaongoza.

  Napenda nianze kupambanua moja kwa moja.

  Nyakati.
  Tanzania ya sasa inahitaji sana uzisome nyakati hizi. Ukweli ni kwamba wananchi wako wengi wameelimika, teknolojia pia imerahisisha mawasiliano. Leo hii ni rahsi sana kujifunza na kuiga mambo yanayofanyika nchi za mbali kwa vile tu watu wanaona kwenye luninga na kusoma kwenye mitandao. Naomba sana uzitambue nyakati hizi ujaribu kuongoza taifa lako kwa kuendana na nyakati.

  Maisha,
  Mheshimiwa rais, maisha ni magumu sana kwetu sisi raia wa chini. hivi unafahamu kuwa wengine tunalala njaa? Hebu fikiria tu kwa haraka haraka "sisi juzi tumelala njaa kabisa, kumbe viongizi wengine walilala hotel ya kulipia Tshs 400,000/=?" Hiyo laki nne tungeipata sisi ingetutoa mwaka mzima.

  Bidhaa zote zimepanda sana, mafuta, sukari, sabuni, billi za umeme n.k, unakumbuka wakati alikuwepo Mh. Mkapa tulikuwa tunanunua kiberiti kwa Tshs 20? unajua kuwa leo kinakimbilia Tshs 200? Wahurumie wanachi wako mheshimiwa! Panua roho ya kusaidia watu.

  Kuwasaidia wanachi wako ni kuwa na mpango madhubuti wa kuhakikisha hata hizi bidhaa zinashuka bei, billi za umeme zinakuwa ndogo. Kwakweli ukifika huku kwetu inasikitisha sana.

  Migogoro.
  Yaani jana nilifikiria sana nikawaza sana, nikafikia hadi kusema kumbe hata mimi naweza kuwa rais na nikalifanya taifa langu kuwa la amani. Mheshimiwa rais, wewe unajisikiaje migogoro inapokuwa mingi nchini mwako?

  Vyuo Vikuu
  Madaktari
  Walimu
  Tatizo la Umeme
  Mauaji ya raia yanayofanywa na polisi,
  Manesi nao wanalalamika,
  Maisha magumu n.k

  Haya yote na mengine mengi yanaisumbua sana hii nchi. Juzi wilaya ya rungwe kulikuwa na maandamano walimu wanambana mkurugenzi wa halmashauri awalipe mishahara yao palikuwa hapatoshi ungekuwepo ungeona kweli kuwa hii nchi inahitaji mtazamo mpya katika uongozi.

  Mheshimiwa Rais, uongozi wako wote kuanzia ngazi za juu (wizara) hadi huku chini kwa kitongozi wa mtaa huduma zake ni mbaya mno. hivi unafahamu kuwa hizi halimashauri zako za Wilaya zimejaa uozo? Unafahamu kuwa sisi wananchi bila kutoa chochote hatuwezi kuhudumiwa? Tukisema tukaripoti Takukuru tunageukwa na kuonekana wabaya ikiwezekana kukosa huduma kabisa?

  Mwananchi anafuatilia leseni ya biashara ili ajitafutie chakula cha kila siku pia alipe kodi TRA kwa faida ya nchi yake, lakini unakuta huyu mtu anazungushwa hadi anakata tamaa je Serikali si imekosa mapato ya bure? Wataalamu wengi husema njia huharibiwa na kiongozi! Rais kama ungekuwa serious na kazi yako hata huku kijijini viongozi wangefanya kazi kwa utii. fikiria haya......  Mwisho,
  Mheshimiwa napenda sana kukuomba utumie moyo wa huruma, kama huna mzigo au wito wa kuiongoza nchi ni bora ukawapatia wengine ili kunusuru maisha ya watanzania wengi na hata wewe utoke kwa amani. Tunakokwenda ni pabaya mno, kama wataalamu wameanza migomo unadhani utaenda kujificha wapi? vumilivu umeisha kwa Watanzania wengi nakuomba rais wangu yafikirie haya.

  HAKUNA KIONGOZI YEYOTE ANAYEWEZA KUFANYA VIZURI ASIPOKUWA NA HOFU YA MUNGU.

  Asante.
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwanini uwe na hofu ya aliyekuumba kama huna makosa? Huo ni ujinga dhahiri kabisa. Inatakiwa uyaogope na uwe na hofu ya makosa na si hofu ya Mungu.
   
 3. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Mkuu tunaposema hofu ya Mungu hili ni neno la kiufundi kwa watu wa Imani wanalifahamu halina maana ya hofu ya kujihofia kwa mabaya lina maana ya ucha Mungu! Yaani ni lazima umtambue Mungu kuwa yupo na umshirikishe kwa kila jambo!
   
 4. f

  fluphenazine Member

  #4
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sikio la kufa halisikii dawa
   
 5. w

  wenyajr Member

  #5
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maana ya kuwa na hofu ya mungu the fear of God i s the begining of wisdom
  ukiwa na hofu ya Mungu unakua na hekima maana anakupa nguvu na hekima ya kuongoza tumwombee maana mambo yako tight tuache porojo kumpiga madongo haisaidii ila anapochemka tumwambie ukweli
  Baba JK Miaka 4 bado unaweza fanya kitu cha maana wanao kusumbua PIGA CHINI Ukicheka nao itakula kwako jenga CV Umalize vizuri
   
 6. R

  Rapture Man JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Serikali iliyoko madarakani inatupeleka kubaya sana. Watu wengi tu wanaona tunakoelekea. Sasa hawa walioko madarakani, ni kweli hawaoni au wanafanya MAKUSUDI? Anyway akina Ghadafi, Mubarak na yule M-tunis waling'ang'ania madaraka, yakawakuta yaliyowakuta. Bashir Assad naye anarudia kosa lile lile. Kwa hiyo si ajabu na hapa TZ wakifanya kosa hilo hilo.

  PASIPO 'KUMWAGA DAMU' (- i.e. kuumia, kujitoa muhanga) HAKUNA UKOMBOZI.
   
 7. S

  Samsindima Member

  #7
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutumie majukwaa kama JF kumshauri Rais kubaini viongozi waovu miongoni mwetu na yale mabaya wanayoyafanya tuyaeleze. Kumekuwa na tabia ya viongozi huku vijijini kulindana na kufichiana madhambi, ukienda kwenye kata na tarafani mambo ni hivyo hivyo. Ukipenya Wilayani au Mkoani utazushiwa zengwe hadi jambo lako life. Kwa utaratibu huu mabaya na maovu hayawezi kumfikia Rais, kwa hiyo njia pekee ni kutumia vyombo hivi vya kijamii kwani naamini Rais anapatiwa yanajitokeza na yanayosemwa. Wasaidizi na washauri wa Rais inaonekana hawampi taarifa zote zinazokera wananchi. Wanazimeza! Viongozi wazuri na wenye weledi na upendo wapo lakini kwa sababu hawana wa kuwabeba na kuwapigia debe ngazi za juu tunajikuta tunabaki na makanyaboya, walaji, wezi na manyang'au wasiojali watu kwa lolote lile. Rais asikilize vilio vyetu asikubali anayoelezwa na washauri wake bila kuyafanyia tathmini. Inabidi kufanya ukaguzi wa watendaji wote na kuwapumzisha wale wote ambao ni wazi
  hawawezi majukumu waliyopewa ama kwa vile wamewekwa kwenye nafasi hizo kwa kubebwa au hawana uwezo.
   
Loading...