Katika dola moja ya kimarekani pana picha ya piramidi ambayo kifuniko chake cha juu ni jicho. Pia kwa juu pana maandishi haya ANNUIT SEPTIS na kwa chini yake pana maandishi haya NUVOS ORDO SECLORUM na chini yake THE GREAT SEAL. Hii nuvos ordo seclorum inasemekana ina maanisha secular order ikiwa na maana non-religious(yaani wasio na dini) cha kukanganya pembeni mwa piramidi pana maandishi IN GOD WE TRUST. Sasa naomba msaada kwa wana JF anaefahamu:-
-Nini maana ya hili neno ANNUIT SEPTIS?
-Kama serikali haina dini kwa maana ya secular order hii tena IN GOD WE TRUST Yaamaanisha kwamba wasio na dini bado hata hivyo wana mungu?
-.Na hii GREAT SEAL huu ni mhuri mkuu wa nini na hii alama ya piramidi asili yake ni nini?
Tafadhalini naomba msaada wenu wachambuzi wa mambo.

Kwa ufupi Marekani ni dola iliyoamua kutengeanisha Kanisa na Serikali (Church and State) kutokana na zahama walizozipata huko Ulaya wakati wa zama za giza (Dark Age). Ila hiyo haimaanisha waliacha Msingi wao wa Ukristo wa Kiprotestanti (Protestant Ethic). Pia ukumbuke kuwa zama hizo Ukristo (Christianity) ulikuwa umekumbatiana sana na dhana ya Ustaarabu (Civilization) ambao ulikuwa ukisambazwa duniani na Ubeberu (Imperialism). Ndio maana walichinja Watu wa Asili ya Marekani wakati wanaingia Marekani. Kisha wakachukua mabibi na mababu zetu utumwani huko Amerika. Hivyo usishangae kuona hizi alama za ajabu kwenye Dola ya Kimarekani, zote zinaashiria kuwa hilo ni taifa lilolijikita katika Udini, Usiri na Ubeberu wa kujaribu kuleta mfumo mmoja wa utawala duniani - A New World Order. Itazame tena hiyo dola utaona neno E pluribus unum, yaani, 'Out of many One'/'Umoja utakanao na Wengi'. Na ile alama ya piramidi lenye jicho ni alama ya Freemasons.
MZEE HUKO UNAKOKWENDA NI MBALI, NI BORA UNGEANZIA NYUMBANI KWANZA; KATIBA YAKO YA TANZANIA INAKWAMBIA SERIKALI HAINA DINI, LAKINI UKIJA KWENYE WIMBO WA TAIFA TUNAIMBA MUNGU IBARIKI TANZANIA,
SWALI LINARUDI PALEPALE NI MUNGU GANI HUYO WAKATI KATIBA INASEMA SERIKALI HAINA DINI, NA WASIO ABUDU MUNGU (KINGUNGE), WANA HAKI GANI YA KUIMBA HUU WIMBO WA TAIFA?
mzee toa kwanza kibanzi ndio utaluiona boroti