Nuru, lugha ya programu ya Kiswahili

AVIC3NNA

Member
Jan 5, 2023
5
13
Nuru ni lugha ya programu ya Kiswahili. Inafanana na lugha zingine kama python na javascript, tofauti ikiwa imetengezwa kwa Kiswahili.

Lugha hii imetengenezwa ili kuwawezesha wazungumzaji wa Kiswahili kujifunza kwa urahisi dhana za programu (programming concepts) licha ya kutojua Kiingereza.

Ni rahisi kujifunza na hutumia maneno ya kawaida ya Kiswahili kama vile "andika()" kuchapisha kitu au "jaza()" kuomba ingizo kutoka kwa mtumiaji. Jumbe zote za makosa (Error messages) pia zimeandikwa kwa Kiswahili ili ziweze kutambuliwa na kusahihishwa kwa urahisi.

Na licha ya hayo yote ni programu ndogo (mb 3 tu) na inaweza kutumika kwenye komputer (Windows na Linux) na simu za Android.

Kujifunza jinsi ya kuprogram ni muhimu katika enzi hii ya kidijitali na Nuru itafanya iwe rahisi kwako kujifunza.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom