Nukuu za ijumaa.......

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
20,051
23,499
BABA NIFUNDISHE KUHUSU
WANAWAKE
"Nikufundishe nini mwanangu
kuhusu wanawake? Baba yako
nimezeeka ghafla nikiwa na
ufahamu mdogo na mwanangu
umeshakua kiasi cha kuhitaji
elimu hii adhimu, nikupe neno
gani?, labda hivi,
1.KUHUSU TAMAA ZAO. -
Mwanamke yeyote anaweza
kukutamani kimapenzi isipokuwa
Mama yako.
2. KUHUSU HULKA ZAO.
-Wanawake wote huonesha
upendo wao waziwazi isipokuwa
wale waliotendwa kabla.
3.KUHUSU KUACHANA.
-Mwanaume kumuacha
mwanamke anayempenda ni
kama simba kuacha kula swala,
Mwanamke kumuacha
mwanaume ni rahisi kama swala
kumkimbia Simba mzee.
4.KUHUSU TABIA.
-Jihadhari na maneno ya vijiweni
kwamba wanawake wote wako
sawa kitabia. No, lakini kumbuka
hakuna Mwanamke asie
Mwanamke.
5. KUHUSU MPENZI WA ZAMANI.
-Kujaribu kumsahau mwanamke
uliyewahi kumpenda ni kama
kumkumbuka mtu usiyemjua. Ni
ngumu.
6. KUHUSU KUOA.
-Muhimu kuoa, na ni ngumu sana
Kumjua mke mwema kabla ya
kuoa, ni waigizaji wazuri sana.
Kumbuka maneno ya Albert. "
Muhimu kuoa, ukipata mke
mwema utakuwa na furaha,
ukipata mke mwovu utakuwa
mwanafalsafa.
7. KUHUSU USALITI.
-Vizuri kujiandaa kisaikolojia
kusalitiwa, la usipojiandaa ama
waweza kuua mtu au hata kujiua.
ukiua mtu maisha yako yatakosa
furaha siku zote, ukijiua
mwenyewe, hao waliokusaliti
wanaweza kuishi kwa furaha
zaidi ya ulivyokuwa hai.
8.KUHUSU PESA NA MAPENZI.
-Mapenzi bila pesa yanapatikana
kwa wingi sana huko mbinguni,
hapa duniani ni ngumu mno,
lakini usihofu sana, kuna
makubaliano bila pesa. Omba
mungu.
9. KUHUSU UONGO.
-Wahenga walisema Ukweli
unauma, Na mimi nakuambia
"Uongo unaua"
10. KUHUSU KUWAJUA
WANAWAKE.
-Ewe mwanangu, kutaka kumjua
mwanamke unahitaji miaka mingi
ya kuishi kuliko idadi ya nywele
zao. Usihangaike na vitabu,
makala, majarida, filamu, nyimbo
na hotuba za wanaofundisha
mandhari za wanawake. Kuna
kanuni moja tu ya kupenda, " ili
ubaki salama katika kupenda
sharti ujipende kwanza".
...Basi mwanangu hayo ndio
machache naweza kukuhusia, na
wewe una nafasi ya kujifunza
zaidi na kufundisha kwa ufanisi
zaidi kuliko Mimi...
Umependa elimu gan hapo??
Shea uwezavyo na wengine.
 
mkuu no 6. ni kweli hawa viumbe kwa kuigiza ni hatari lkn ni muhimu sana kumshirikisha muumba wako ndipo unaweza kupata mke mwema
 
Aisee nimeipenda sana kwani kwa 100% ni kweli tupu! Hata Mungu anajua hilo ndio maana alituasa kuwa 'wanawake ni mama zenu ILA ishini nao kwa akili! Unajua kwanini? Wanawake waliwaharibu hadi manabii wake.
1. Hawa ndie alimlaghai Adam
2. Delila kwa Samson
3. Mke wa Habibu ' bado unamtegemea huyo Mungu wako?'
Mifano ni mingi mno mno.
 
N
Aisee nimeipenda sana kwani kwa 100% ni kweli tupu! Hata Mungu anajua hilo ndio maana alituasa kuwa 'wanawake ni mama zenu ILA ishini nao kwa akili! Unajua kwanini? Wanawake waliwaharibu hadi manabii wake.
1. Hawa ndie alimlaghai Adam
2. Delila kwa Samson
3. Mke wa Habibu ' bado unamtegemea huyo Mungu wako?'
Mifano ni mingi mno mno.


Mkuu ndio maana waliitwa HAWA..
Yaani hawaelewei,hawaaminiki,hawashikiki,hawana maana..na kuendelea
 
Mie nakubaliana na 2. Lkn uleti uzi wa wanaume pia maana sie mshatujua ingekuwa vizuri na nyie tukawajua.Ila mbona moja umelisahau WANAWAKE NI WAVUMILIVU SANA.
 
Back
Top Bottom