"Mmechaguliwa na maelfu ya watanzania kuingia bungeni, lakini mambo mnayofanya hayaendani kabisa na hadhi yenu," alisema Makinda huku baadhi ya wabunge wakimzomea na wengine kushangilia"
Kwa kauli kama hiyo, hivi sasa alipaswa awe amekwisha achia ngazi ngazi "kung'atuka" kutoka katika kiti cha USPIKA.
Tafsiri rahisi ya maneno hayo ni kwamba BUNGE limemshinda, kwa kuwa yeye kama "KIRANJA MKUU", ameshindwa kudhibiti nidhamu ya BUNGE na WABUNGE.
Nina amaini kabisa kuna miongozo na sheria zilizo wazi juu ya wakiukaji wa vifungu hivyo, ila ile dhana ya kuogopana na kuoneana haya ndio imewafikisha hapo.