kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
KATIKA hotuba yake iliyokuwa na kurasa 21 na maneno yapatayo 9,853 ya kuahirisha Bunge la Bajeti lililokaa kwa takribani siku 73 mjini Dodoma, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alizungumza mambo mengi kwa kirefu.
Zifuatazo ni baadhi ya nukuu muhimu katika hotuba hiyo.
• Mkutano wa Bunge uliomalizika umejadili na kupitisha Bajeti ya Kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa ufanisi mkubwa. Bajeti hii ni ya kihistoria kwa sababu kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru mwaka 1961 imetenga asilimia 40 ya Bajeti ya Sh trilioni 29.5 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
• Mijadala ilikuwa yenye msisimko na wakati mwingine ikiambatana na hisia kali kwa baadhi ya wabunge kutokana na hoja ambazo zililenga kujenga na kuiletea maendeleo nchi yetu.
• Azma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kila Shilingi inayokusanywa kupitia kodi za wananchi, mikopo na michango ya Wahisani inatumika katika shughuli iliyokusudiwa na lazima thamani ya fedha (value for money) ionekane bayana.
• Vipaumbele katika mpango wa mwaka huu ni pamoja na kutenga fedha nyingi zaidi katika sekta za elimu, afya, maji, kilimo, viwanda, miundombinu, uchukuzi, bandari, usafiri wa anga na majini, maliasili, nishati na madini.
• Katika Mkutano wa Bunge uliomalizika upinzani ulijenga taswira potofu bila mafanikio kwa wananchi na jumuiya ya kimataifa kwamba kuna kuminywa kwa demokrasia ndani ya Bunge.
• Katiba imetoa haki na kinga kwa wabunge kujadili na kuhoji utendaji wa serikali kwa uhuru bila mashaka ya kushitakiwa wakiwa bungeni. Kinga hiyo haijatolewa nje ya bunge, hivyo mbunge hajafungwa mdomo labda aamue kujifunga mdomo mwenyewe.
• Wabunge waliosusa Bunge watafakari upya uamuzi wao. Watumie busara zao waingie bungeni ili watoe ushauri kwa Serikali ambao utaliletea Taifa letu maendeleo.
• Bunge letu linaongozwa na Katiba, Sheria na Kanuni za Kudumu za Bunge, hivyo ni vyema kila mbunge akazifuata ili kuondoa manung’uniko yasiyo ya lazima.
• Wabunge na wananchi washirikiane na Serikali, kila mmoja kwa nafasi yake, kutekeleza mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021.
• Hatua za kibajeti na kisera zitakazotekelezwa na Serikali katika mwaka ujao wa fedha ni; mosi, kuimarisha usimamizi wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali na umuhimu wa kila mwananchi kulipa kodi. Pili ni kudhibiti matumizi ya fedha za umma.
• Serikali itaendelea kuzingatia maoni na ushauri wa wabunge katika kuendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato na kupanua wigo wa kodi.
• Watendaji wakuu wa wizara, wakala, idara zinazojitegemea, mashirika na taasisi za umma, mikoa na halmashauri zote nchini wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanasimamia vizuri ukusanyaji wa mapato na kuwepo kwa udhibiti wa kutosha wa matumizi ya fedha za Serikali.
• Serikali ya Awamu ya Tano haitasita kuchukua hatua stahiki kwa viongozi wa umma au watumishi wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma. Kuzingatia maadili siyo suala la hiari bali ni lazima.
• Kupambana na ufisadi si nguvu ya soda bali suala endelevu. Mbali na hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa za kutumbua majipu, serikali imeanzisha Mahakama Maalumu ya kushughulikia makosa ya rushwa na ufisadi.
• Serikali pekee haiwezi kufanikiwa vita dhidi ya ufisadi na maovu mengine kama wananchi na wadau wengine hawataiunga mkono katika jitihada zake za kupambana na vitendo hivyo. • Hakuna kufungua maeneo ya starehe (Bar na pubs) wakati wa muda wa kazi ili vijana na watu wengine waende kufanya kazi kwa maendeleo yao na Taifa.
• Hali ya chakula nchini ni ya kuridhisha na matarajio ya uzalishaji kwa msimu wa 2015/2016 ni mzuri. Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ijipange vizuri kununua mahindi yatakayozalishwa na kuanzisha vituo vya ununuzi karibu na wananchi.
• Sukari ya kutosha imeingizwa nchini kufidia upungufu. Kwa bahati mbaya, bado soko la sukari limeendelea kuyumba kutokana hisia tu kuwa sukari iliyopo haitoshi na kusababisha bei kuwa juu. Serikali itaendelea kusimamia kushuka kwa bei ili mlaji wa chini amudu kuinunua.
• Ili kumaliza tatizo la sukari, tathmini mpya inafanyika ili kujua mahitaji halisi ya sukari, viwanda vilivyopo kuongeza uzalishaji na kuwa na mkakati wa kuanzisha viwanda vipya vya sukari pamoja na kupunguza gharama za uzalishaji.
• Dhima ya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano wa Mwaka 2016/2017 – 2020/2021 ni kuanza ujenzi wa Taifa lenye Uchumi wa Kati unaoendeshwa na viwanda ifikapo mwaka 2025.
• Uzoefu na historia ya nchi nyingine unaonesha kwamba ujenzi wa uchumi wa viwanda utaliweka Taifa letu katika kundi la mataifa yanayozalisha bidhaa bora na zenye ushindani wa soko la kimataifa badala ya kuwa chanzo cha malighafi na soko la bidhaa kwa viwanda vya mataifa mengine.
• Serikali ya Awamu ya Tano katika kutekeleza mpango wa viwanda inaipa sekta binafsi jukumu la ujenzi na uendeshaji viwanda na biashara nchini na Serikali inabaki na jukumu la kuweka mazingira wezeshi na rafiki ya kufanya biashara na uwekezaji.
• Wananchi na Watanzania wote wanatakiwa kutambua fursa zilizopo kwa kubaini sehemu ambayo kila mmoja anaimudu katika mnyororo wa manufaa ya ujenzi wa uchumi wa Kati.
•Mamlaka za mikoa na wilaya lazima zitenge maeneo kwa shughuli za viwanda na biashara.
• Ushirika umeendelea kuwa sekta muhimu katika maendeleo ya jamii, kujenga uchumi wa wanachama na kuchangia pato la taifa. Serikali itahakikisha Sheria ya Ushirika Na. 6 mwaka 2013 inang’ata na kuainisha hatua kali ambazo zitachukuliwa dhidi ya wale wote wanaokiuka Sheria hiyo.
• Wananchi na wakazi wote wa Dar es Salaam watoe ushirikiano katika kutunza miundombinu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka.
• Serikali imeanza mchakato wa Mpango wa ujenzi wa Awamu ya Pili na Tatu wa mabasi yaendayo haraka katika barabara za Mbagala na Gongo la Mboto, Dar es Salaam ili wananchi wa maeneo hayo waanze kufaidi huduma hizo.
• Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuyapatia maeneo yaliyo nje ya Gridi ya Taifa nishati bora ikiwa ni pamoja na maeneo ya visiwa. Wakala wa Usambazaji wa Umeme Vijijini (REA) inakamilisha taratibu za uendeshaji kwa waendelezaji wa mini-grids. Taratibu hizi zinategemewa kukamilika mwezi huu ili kuweza kushindanisha waendelezaji wa mini-grids, micro-grids na solar home systems.
• Mpango wa elimu bure umeongeza asilimia 10.74 ya wanafunzi 877,489 walioandikishwa mwaka 2015. Lakini mpango una changamoto za upatikanaji wa miundombinu, samani pamoja na uelewa wa jamii juu ya wajibu wao kuhusu dhana ya elimu bila malipo.
• Katika kuchangia madawati, shule za msingi zimepata madawati 2,632,392, sawa na asilimia 77 ya mahitaji wakati shule za sekondari zimefikisha madawati 1,395,138 sawa na asilimia 93 ya mahitaji.
• Ili kuhakikisha utoaji wa mikopo ya elimu ya juu unafanyika kwa ufanisi; Serikali itabadilisha utaratibu wa kupanga na kutoa mikopo ili kuwafikia wanafunzi wote wenye uhitaji zaidi wakiwemo yatima na wenye uwezo mdogo kiuchumi bila kujali aina ya programu wanazozisoma. Serikali inaendelea kufanya maboresho ya kimfumo na kisheria ili kuimarisha urejeshwaji wa mikopo.
• Ili kuhakikisha ukuaji wa sekta ya elimu unaambatana na ubora stahiki na kukidhi mahitaji ya sasa, Serikali itafanya mapitio na kuhuisha Sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na Vyuo Vikuu Nchini, kuimarisha mfumo wa ki-elektroniki wa udahili wa pamoja (Central Admission System) pamoja na kuendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na kuchukua hatua kali kwa taasisi zote za elimu zinazokiuka taratibu zilizowekwa.
• Kwa ujumla hali ya usalama wa raia na mali zao ni shwari pamoja na matukio ya kihalifu yaliyotokea katika Mikoa ya Tanga, Geita, Mwanza, Mara na Dar es Salaam. Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama ikiwemo Jeshi la Polisi imechukua hatua za haraka kwa kufanya operesheni maalumu zilizowezesha kubainika na kukamatwa kwa baadhi ya watuhumiwa.
• Bado tunalo jukumu la kila mwananchi kushiriki katika masuala ya ulinzi na usalama wa nchi yetu. Tushirikiane kubaini matukio yoyote yanayoashiria uvunjifu wa amani na usalama wa raia.