Nukuu 25 za wanafalsafa maarufu ulimwenguni

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
735
1,464
1. "Napenda kuwaambia wale wanaodhani siasa haiwahusu, Moja ya madhara ya kukataa kujihusisha na siasa ni kwamba utaongozwa na watu uliowazidi akili. Na kwa upungufu wao wa akili watafanya maamuzi ya kila kitu kinachohusu maisha yako"- Plato.

2. "Moto mkali zaidi wa jehanam wameandaliwa wale wanaojifanya wapo neutral mahali ambapo wanyonge wanaonewa"- Martin Luther King, Jr.

3. "Kama hatuamini uhuru wa maoni kwa wapinzani wetu, basi hatuamini katika uhuru wa maoni kabisa. Kwa sababu wafuasi wetu hawahitaji uhuru wa kusema, bali wapinzani wetu"- Noam Chomsky.

4. "Binadamu kwa asili ni mnyama wa kisiasa. Kumtenganisha na siasa ni sawa na kumzuia kuishi"- Aristotle.

5. "Changamoto kubwa ya ulimwengu kwa sasa ni kwamba wenye akili hawataki kujihusisha na siasa, na hivyo wajinga wamepewa mamlaka ya kuwatawala wenye akili na wasio na akili"- Donald Trump.

6. "Siamini kama tofauti ya mawazo katika siasa, au imani ya kidini inaweza kupoteza urafiki wangu na mtu yeyote"- Thomas Jefferson.

7. "Wanaosema dini na siasa havina uhusiano, hawajui maana ya dini"- Mahatma Gandhi.

8. "Siasa ni sanaa ya kuibua matatizo ya jamii, kuonesha unaumizwa nayo, kisha kujifanya unayatatua kumbe unayaongeza. Maana bila matatizo ya jamii hakuna wanasiasa"- Groucho Max.

9. "Siasa ni vita isiyo na damu, na vita ni siasa yenye damu"- Mao Tse Tsung.

10. "Sipendi vichekesho (comedy), lakini napotaka kucheka hufuatilia namna serikali inavyofanya mambo yake"- Will Rogers.

11. "Ni afadhali kuwa na jeshi la kondoo linaloongozwa na Simba, kuliko jeshi la simba linaloongozwa na kondoo."- Napoleon_Bonaparte.

12. "Lengo la kwanza la vita sio kufa kwa ajili ya nchi yako, hapana. Bali ni kuua mtu mwingine kwa ajili ya nchi yake."- George_Patton.

13. "Lazima nisome siasa na vita ili mwanangu apate uhuru wa kusoma hesabu na falsafa."- John_Adams.

14. "Washindi wanashinda kwanza halafu wanakwenda vitani, wanaoshindwa huenda vitani kwanza halafu ndio wanatafuta ushindi."- Sun_Tzu.

15. "Inafahamika vizuri katika vita, majeruhi wa kwanza ni ukweli. Kwamba, wakati wa vita, ukweli huharibiwa vibaya na propaganda."-
Harry_Browne.

16. "Propaganda ikitumiwa vizuri inaweza kumfanya mtu aone kuwa paradiso ndio jehanam na jehanam ndio paradiso."- Adolf_Hitler.

17. "Mtu mwenye ufahamu wa kweli, si tu kwamba atawapenda maadui zake wanapofanya vizuri, bali pia atawachukia marafiki zake wanapokosea."- Friedrich_Nietzsche.

18. "Madaraka ni kama mchanga. Jinsi unavyoyakumbatia kiganjani ndivyo yanavyokuponyoka."- Confucus.

19. "Tofauti kati ya akili na ujinga ni kuwa, akili ina kikomo, ujinga hauna kikomo."- Albert_Einstein.

20. "Kuna watu wawili tu wasioweza kubadili mawazo. Mpumbavu kuliko wote na mwenye hekima kuliko wote."- Plato.

21. "Rais ni mtu wa kushutumiwa kila mara. Ukiona hataki kushutumiwa, ujue hajui sababu ya kuwa hapo."- Harry_Truman.

22. "Sote tumezaliwa wajinga, tunahitaji bidii kidogo ili kuwa na maarifa, au bidii kubwa sana ili kuendelea kubaki wapumbavu. Baadhi huchagua njia ya pili."- Benjamin_Franklin.

23. "Unajisi wa sheria hutokea pale ambapo mahakimu/majaji, hujiweka mikononi mwa watawala na kuamini watawala wana nguvu kuliko sheria"- Lamar_Smith.

24. "Kuliko kuwapa wanasiasa ufunguo wa maisha yako, ni bora ubadili kitasa"- Doug_Larson.

25. "Mpumbavu akipewa nyundo hudhani kila tatizo anaweza kulitatua kwa nyundo" .-Nelson Mandela

JE WEWE UPO UPANDE UPI?
 
Umasikini na uharibifu wa mazingira ni watoto mapacha na mama yao ni ujinga
Rais Mwanyi
 
hata mimi ni mfungwa mtarajiwa,ndio maana leo nimekuja kuwatembelea.teheteheee
 
"Sote tumezaliwa wajinga, tunahitaji bidii kidogo ili kuwa na maarifa, au bidii kubwa sana ili kuendelea kubaki wapumbavu. Baadhi huchagua njia ya pili."- Benjamin_Franklin.
 
"Madaraka ni kama mchanga. Jinsi unavyoyakumbatia kiganjani ndivyo yanavyokuponyoka."- Confucus.
 
Back
Top Bottom