Ntagambi.....29

0713417189

Senior Member
May 12, 2021
108
196
NTAGAMBI.......19
Mtunzi; Lovi Pius Kijogoo.
0757 238 304.( WHATSAP )

Tanga.


SEHEMU YA KUMI NA
TISA..
( 19 )

ILIPOISHIA......
Alipoinua kichwa Ntagambi, kwa mbali aliona Jengo la mfalme. Alilia sana, huku akijisemea mwenyewe kwamba, "Sasa nimekwisha". Zilibaki kama mita mia wafike, Ila mbele kidogo alionekana binti akiwa ameificha sura yake kwa kutumia blauzi yake. Ndani ya sidilia zilionekana titi changa zilizochongoka mithili ya mdomo wa kuku. Tumbo lake dogo lililotuna kwa mbele kiasi, mkono wake wa kuume alikuwa ameshika panga. Naam je ni nani huyo na analengo gani.

ENDELEA NAYO.....
Hatimaye walifika aliposimama huyo Binti. Hakuwa na muda wa kuzungumzwa, zaidi ya kutekeleza kilichomleta eneo ilo. Aliuweka upanga wake sawa, akaruka juu na kutua kwenye kichwa cha askari mmoja. Akaanza kutembeza panga kwenye miili ya askari hao. Sekunde kadhaa zilitosha kuuchafua uwanja huo. Mikono, miguu ilidondoka chini pasi huruma na damu zikimwagika kwa kasi ya ajabu.

Binti huyo alijeruhiwa mkono, akachukuwa kitambaa na kulifunga jeraha kisha akaendelea kupambana. Ntagambi alikuwa ameshikiliwa na askari akiwa hoi bin taaban. Alipojaribu kuyafumbua macho yake alishindwa, yalivimba sababu ya kipigo na kulia sana.

Binti huyo aliposikia sauti ya mtoto akilia, miongoni mwa askari hao. Alizidi kuchanganyikiwa, hasira zikampanda mpaka kufika kikomo. Akabadilisha aina mapigo, sasa akawa anakupiga panga la kwanza, akirudia la pili anahakikisha amekumaliza kabisa. Askari walijuta, wakatamani ardhi ipasuke wakajifiche huko, lakini haikuwezekana.

Hatimaye binti huyo, alimuona askari aliyembeba mtoto. Vita ikaanza upya watu walikatwa shingo kama ng'ombe. Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika, pigano la wababe wenye kulijua panga vyema nalo likiwatii, bila ya kukaidi amri.

Kiongozi wa askari hao, alikuwa mikononi mwa binti huyo akiwa amewekewa panga katika shingo yake. Muda wowote shingo hiyo ingelitenganishwa na kiwiliwili. Ntagambi alipoinua kichwa chake na kumtazama yule binti kwa makini akagunduwa ni Chidumu, binti mfalme.

Upande wa pili askari nae, alikiweka kisu katikati ya tumbo la mtoto. Hapa sasa ilikuwa chagua moja kunyoa au kusuka. Askari huyo aliongea maneno ya vitisho. Walikuwa wameshagundua kwamba huyo mtoto ni wa binti mfalme, na ndiye wanaepambana nae hapo.

"Weka panga chini, tukuchukue mpaka kwa mfalme. Tumehangaika sana, usiku na hata mchana kukutafuta wewe" alizungumza askari aliyemuwekea mtoto kisu. Chidumu hakujibu, alikaa kimyaa. Huku akiwa amemkazia macho Askari huyo. Kama alikuwa anafanya mahesabu makali katika kichwa chake, namna ya kumnasua mwanaye.

"Unaleta ujeuri hutaki kujibu eeh! sasa namtoboa tumbo huyu mtoto" alifoka kwa hasira askari huyo. Chidumu alionekana kama machozi yanameremeta machoni kwake. Akayang'ata meno yake kwa hasira na uchungu. Kisha akazungumza, "Ukithubutu kufanya hivyo, utaibeba Dunia katika mabega yako"

Kauli hiyo ilimchukia sana askari huyo. Akaanza kuhesabu moja mpaka tatu ili ammalize mtoto. Ile anaenda kutamka tatu alishtukia upanga unatuwa katika mgongo wake. Alikuwa ni Ntagambi aliweza kumthibiti askari aliyekuwa amemshikilia. Akafanikiwa kuurusha upanga ukafika vyema kama alivyouelekeza. Ntagambi aliwahi akamdaka mtoto na kuanguka nae mpaka chini.
Chidumu akamchinja yule kiongozi wa askari, akahakikisha kichwa kimeanguka pembeni. Ntagambi akiwa pale chini hakuweza kuamka maumivu yalimzidia.

"Mpenzi wangu nakufa!" ilikuwa ni sauti hafifu kutoka kwa Ntagambi. Chidumu alichanganyikiwa akashindwa aanze kumsaidia yupi, mtoto alikuwa ana Hali mbaya, njaa ilimzonga akajaribu kumnyonyesha. Lakini mtoto hakuwa hata na uwezo wa kuzivuta chuchu. Chozi likamtoka Chidumu. Akazikamua chuchu zake na kumdondoshea mtoto maziwa kinywani mwake.

Askari waliobaki walikimbia, na kwenda kutoa taarifa kwa mfalme aongeze askari wengine. Chidumu akachukua farasi aliyekuwa akitumiwa na askari hao. Akajitahidi akambeba Ntagambi na kumkarisha juu ya farasi. Kisha akambeba mwanaye, wakapanda na kuanza safari alisogea mbele kidogo, akawashusha na kuanza kuwapa matibabu.

Ntagambi kwa mbali alianza kupata ahueni. Akamtazama mpenzi wake usoni takribani dakika tano. Akatikisa kichwa kwa huzuni, huku chozi likimchuruzika katika jicho lake la upande wa kulia. Mtoto hali ilizidi kuwa mbaya. Alikuwa akizivuta pumzi kwa shida kana kwamba kakabwa katika shingo yake.

"Tumeikosea nini sisi Dunia!" Ntagambi alihoji lakini Chidumu hakujibu neno lolote lile. Akili yote iliishia kwa mwanaye aliyekuwa akiupigania uhai wake kwa mara ya mwisho.
Mtoto alianza kukoroma, kuvuta pumzi ilikuwa ni mtihani mzito kwake. Anahangaika huku na kule akayafumba macho yake, akawa ameikamilisha safari yake ya hapa Duniani, angali akiwa bado mtoto mchanga kabisa.

Kilio kilitawala si Ntagambi, si Chidumu. Walianguka kilio cha simanzi. Chidumu akawa anamtikisa mwanaye akijua labda kalala, "Mwanangu, kipenzi changu, damu yangu. Amka mwanangu, nimehangaika kwaajili yako, nilikuwa tayari kufa kwaajili ya kuutetea uhai wako. Nimeyaacha majumba ya kifalme kwaajili ya kuishi nawe pamoja na Baba yako. Lakini wewe umeamua kuniacha sawa mwanangu!. Nenda mwanangu! umeona ni vyema kuniacha peke yangu. Tumbo linauma! tumbo la uzazi laniuma mwenzenu! Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii." alitowa yowe la uchungu Chidumu. Maumivu, mawazo yakauzonga mwili wake. Kuzungumza akashindwa akabaki analia tu kama mtoto.

Ntagambi nae ni kama alikuwa amechanganyikiwa. Alikuwa akiuzunguka mwili wa mwanaye kutoka kushoto kwenda kulia, na kutoka kulia kwenda kushoto. Huku machozi yakiwa yanamdondoka. Hakika moyo wake ulikuwa katika mateso na maumivu makali sana.

Wakiwa bado wamezama katika lindi ilo la simanzi. Kwa mbali walisikia vishindo vya watu wakiwa wanatembea. Alipoinua kiichwa Ntagambi alishuhudia jeshi kubwa likiwa linakuja na silaha nzito. Katu hakuwahi kushuhudia idadi kubwa ya askari kama hiyo, mfalme aliomba msaada katika falme za jirani.

"Hakika mfalme kaamua, sijui kama tutasalimika" alijisemea kimoyomoyo Ntagambi. Waliamua wachimbe kaburi hapo hapo wamzike mtoto wao, Kisha wakimbie. Mwanzo Chidumu aligoma katakata mwanaye kuzikwa hapo. Aliamini mtoto kalala tu, huenda huko mbele ya safari anaweza kuamka. Ni kitu ambacho hakikuwa na ukweli wowote ule. Walikimbizana na muda. Walipomaliza kumzika mtoto, Chidumu alilia sana huku akiwa anazungumza,

"Kweli leo nakuacha peke yako! kwa kheri mwanangu. Nenda pacha wangu, labda ipo siku tunaonana tena" alizungumza Chidumu akiwa analipungia mkono wa kwa kheri kaburi la mwanaye.

ITAENDELEA..........
 
Back
Top Bottom