NSSF yaomba msamaha kodi

NSSF yaomba msamaha kodi

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,716
Reaction score
9,051

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeiomba serikali itoe msamaha wa kodi kwa vifaa na huduma zinazotolewa kwenye uwekezaji wa viwanda.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara.

Aidha, NSSF imesema kuendelea kutoa msahama kwa wawekezaji wengine na kuiacha kando mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo ni sehemu ya serikali, ni kukwamisha kufikiwa kwa uchumi wa kati na maendeleo ya viwanda.

Serikali imepania nchi ifikie uchumi wa kati, wa viwanda, ifikapo 2025.

Akiwasilisha mada kwenye mkutano wa wadau uliomalizika mjini Arusha mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara, alisema kuwepo kwa kodi kumesababisha mtaji kuwa mkubwa na kugharimu mfuko.

Katika wasilisho la mada ya 'Mifuko ya Hifadhi na Viwanda' lililofanywa kwa niaba yake na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Mkulazi, Radhia Tambwe, alisema kama ambavyo msamaha huo umetolewa kwa wawekezaji wa sekta binafsi ni vyema serikali ikaifikiria mifuko hiyo, ili ifanye kazi kwa urahisi zaidi.

“Kuendelea kutoza kodi hii kwetu tunaona itapunguza mapato," alisema Mkurugenzi huyo wa NSSF. "Serikali inaweza kutoa msamaha maalum kwa muda maalum, mfano watupe miaka miaka mitano (na) tukianza uzalishaji kwenye viwanda watutoze kodi hiyo.”

Prof. Kahyarara alisema changamoto nyingine wanayoomba serikali kuiangalia kwa kina ni urasimu ulipo katika sheria ya manunuzi ambayo huchelewesha na kukwamisha shughuli kufanyika kwa kasi inayotakiwa.

“Taratibu za manunuzi ni za muda mrefu, zinapunguza kasi ya uwekezaji kwenye viwanda," alisema. "Hii ni changamoto kubwa sana kwetu.”

Alisema hifadhi ya jamii ni ya umma, lakini wawekezaji wa viwanda asilimia kubwa ni binafsi ambao hawatakiwi kufuata taratibu za manunuzi na hivyo kufanya uwekezaji kwa haraka na kupiga hatua kubwa kimaendeleo.

“Unashindana na anayekwenda dukani moja kwa moja, wakati wewe una taratibu za manunuzi ambazo zinakufanya usubiri kwa muda mrefu.”

Kwa mujibu wa Profesa huyo, kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa teknolojia nchini na wakati mwingine kulazimika kuzitafuta nje ya nchi, na kutaka kuwapo ushirikiano baina ya taasisi za ndani.

Mkurugenzi huyo, alisema NSSF katika miradi mbalimbali ya uwekezaji inatumia wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Sokoine (Sua) na wengineo ambao wamesaidia kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, uwekezaji kwenye viwanda siyo jambo geni kwa kuwa duniani kuna mifuko ya hifadhi ya jamii imefanya hivyo kwenye maeneo ya afya, miundombinu ya barabara, madaraja na nyumba.

Alitolea mfano wa mfuko wa GEPF Afrika Kusini, ambao ni mfuko wa tano kwa ukubwa duniani.

Alisema mfuko huo una wanachama milioni 1.2, unalipa mafao ya pensheni kwa wastaafu 360,000 na una rasilimali za Sh. trilioni moja, huku ukichochea maendeleo ya nchi hiyo.

Mhadhiri wa UDSM, Idara ya Uchumi, Prof. Humphrey Moshi, alisema duniani hakuna sekta muhimu zaidi ya viwanda na nchi zote zilizoendelea ziliwekeza kwenye viwanda.

Prof. Moshi alisema pamoja na kwamba sekta binafsi ni injini ya uchumi, lakini matairi ni serikali ambayo haitakiwi kubaki nyuma.
Alisema kwa miaka 20 ambayo serikali ilikuwa imejiondoa hali ilikuwa mbaya hivyo inavyorudi sasa siyo jambo la kushangaa.

“Tumeishi kwa kuamini ushauri mzuri ni kutoka nchi za Magharibi, lakini ikumbukwe wakati Ulaya inatoka kwenye umaskini na kuingia kwenye viwanda hakuna anayeishi dunia hii aliona hilo," alisema Prof. Moshi.

"Ni miaka 100 hadi 150 iliyopita, tulisoma kwenye vitabu kama historia, leo wanatudanganya.” A
lisema.

CHANZO: Nipashe
 
Ni kweli kabisa. Kama Acacia/Barrick wamesamehewa 99.84% ya kodi waliyokuwa wanadaiwa (kutoka $194,000,000,000 hadi $300,000,000), basi walau kampuni za wazawa zisamehewe pia
 
Back
Top Bottom