Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 137,639
- 272,442
Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya utendaji kazi wa NSSF kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015 .
Ripoti ya NSSF kwa mwaka wa fedha 2014/2015 iliwasilishwa kwa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali ( PAC ) mapema mwaka huu na Mkurugenzi mkuu wa NSSF , Profesa Godius Kahyarara .
=======
Kwa mujibu wa taarifa ya utedaji kazi wa NSSF kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015, ambayo Nipashe inayo nakala yake, shirika hilo lilitumia jumla ya Sh. bilioni 10.1 kulipa posho ya safari kama moja ya vipengele vya gharama za uendeshaji katika mwaka ulioishia Juni 2015.
Kiasi hicho kilikuwa ni ongezeko la Sh. bilioni 1.05 kulinganisha na mwaka uliotangulia.
Ripoti ya NSSF kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015 iliwasilishwa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) mapema mwaka huu na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara.
Prof. Kahyarara aliteuliwa na Rais John Magufuli kuongoza shirika hilo Machi 19 mwaka huu, hata hivyo, akiziba pengo la Dk. Ramadhani Dau ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Februari na sasa ni balozi nchini Singapore.
Utenguzi wa nafasi ya Dk. Dau ulikuja siku chache baada ya taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuonyesha palikuwa na ukiukwaji wa taratibu katika miradi kadhaa ya NSSF.
Tangu aingie madarakani mwaka mmoja uliopita, Rais Magufuli amejipambanua kama kiongozi 'mchumi' na matumizi ya kawaida yameondolewa katika bajeti ya serikali ya mwaka huu.
Taarifa ya utendaji kazi kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015 hiyo ambayo Nipashe inayo nakala yake inaonyesha kwa ujumla, katika uendeshaji wa shirika hilo kwa mwaka huo, NSSF ilitumia jumla ya Sh. bilioni 110, yakiwemo malipo ya Sh. bilioni 26.4 za mishahara.
Pia NSSF ililipa malipo ya kufanya kazi kwa muda wa ziada (overtime), ya jumla ya Sh. bilioni 2.3 na Sh. milioni 97.6 kulipa vibarua.
Semina na masuala kama hayo yaligharimu shirika hilo jumla ya Sh. bilioni 3.3, taarifa ya utedaji kazi hiyo inasema.
Ripoti hiyo inaonyesha pia licha ya NSSF kuwa na majengo yake karibu kila mkoa nchini, ililipa Sh. bilioni 1.3 kama kodi kwa ajili ya ofisi.
Aidha, Sh. bilioni 7.02 zilitumiwa na NSSF kama ruzuku kwa ajili ya gharama za makazi kwa wafanyakazi hao.
WAKURUGENZI SITA
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ipo katika hatua za mwisho kukamilisha uchunguzi dhidi ya waliokuwa wakurugenzi wa idara sita za Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Valentino Mlowola, Mkurugenzi wake aliiambia Nipashe miezi miwili iliyopita.
Mlowola ambaye ni Kamishna wa Polisi alikuwa akizungumza na Nipashe mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa Mahakama ya wilaya, uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa mjini Kibaha.
Wakurugenzi hao walisimamishwa na bodi ya NSSF chini ya uenyekiti wa Profesa Samweli Wangwen Julai kwa tuhuma kadhaa, ikiwemo matumizi mabaya ya ofisi.
Mbali na wakurugenzi hao, bodi hiyo iliyokaa Julai 15 pia iliwasimamisha mameneja watano na mhandisi mmoja.
Waliosimamishwa ni Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi, Yacob Kidula, Mkurugenzi wa Fedha, Ludocick Mrosso na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Chiku Matessa.
Wengine ni Mkurugenzi wa Udhibiti Hasara na Majanga, Sadi Shemliwa, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Mahesabu ya Ndani, Pauline Mtunda na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Crescentius Magori.
Mameneja waliosimamishwa ni Meneja wa Utawala, Amina Abdallah, Meneja wa Uwekezaji, Abdallah Mseli na Meneja wa Miradi, Mhandisi John Msemo.
Wengine ni Mhasibu Mkuu, Davis Kalanje, Meneja Kiongozi kwa mkoa wa Temeke, Wakili Chedrick Komba na Meneja Mradi, Mhandisi John Ndazi.
Uamuzi huo wa kuwasimamisha watendaji hao ulichukuliwa kutokana na taarifa za ukaguzi wa hesabu na shughuli za uendeshaji wa mfuko huo.
Chanzo: Nipashe