NSSF ndani ya ufisadi mzito: Wajanja wapiga zaidi ya Sh. Bilioni 179

Kwahiyo serikali ikimfungulia Dau kesi maana serikali inapigwa chini dk 0?
Daaah, watu hatari hawa.
 
Na hiyo kampuni ya Azimio ichunguzwe utakuta kuna mikono ya wakubwa kwani pembeni ya mradi hapa Usa-River kuna shamba la kiongozi mmoja wa bunge la sasa inawezekana aligawiwa ili asipeleke kamati za bunge huko.Mheshimiwa Zito amepata kigugumizi?Mbona kimya? Naona kamati yake haikuona haya.
 
Hivi hizi ripoti za CAG kipindi cha mkwere hazikuandika haya? Au zilikuwa zinapelekwa kwa JK aziharirir kwa maslahi yake binafsi ndio zinapelekwa bungeni? Hizi hela zilizochezewa na NSSF tu ni hatari kuliko uozo wa bandari? Jamani halafu wastaafu wafia stendi kufuatilia malipo yao kwa ahadi za njoo kesho, hii ni jambo la kupandisha watu kizimbani kabisa.
 
Hiyo ni intressant

http://s07.jamiiforums.com/mini/uyE8/bg_000000/txt_000000/border_000000/flags_0/
 
Dah! Hilo shamba lenu tamu, yaani mabilioni yanatajwa utadhani kama maigizo kumbe kweli. Japo niliona kwenye gazeti mtu wangu fulani huko kaketishwa kwenye bench Kisutu, ametuhumiwa kwa ufisadi. Magufuri ana kazi ya ziada maana naona kama hajui kwamba Watanzania wa sasa sio wale wa wakati wa Nyerere, hawa wanakutafuna kama bado uko hai.

Yaani watu wanapiga hela ndefu wakati akina MOTOCHINI wamezubaa mitaani.
 
Aisee huku kwetu bora aisee, huko kwenu Kenya ndipo hatari tupu, cha ajabu hata kuchukuliwa hatua hamna kwa sababu ya ukabila.

Mkifanikiwa kuanika uozo wa Kenya hivi mtakuwa mmpeiga hatua kubwa sana.

Nmejaribu kupitia Gazeti la Daily Nation yaani mpaka nimechoka, Kenya inanuka.

Njooni mjifunze Tanzania jnisi ya ku deal na rushwa na ufisadi, acheni kujificha chini ya katiba wakati watu wanatafuna nchi mchana kweupee
 

Naona kama unakaririshwa mambo na kuyafuata kama kipofu, hatua muhimu zimechukuliwa dhidi ya ufisadi hapa kwetu. Gazeti la Nation litakuchanganya kwa ajili ya lugha, labda usome Taifa Leo.

Sasa hivi mawaziri watano na makatibu wao wamefutwa kazi na kuburuzwa kotini, pia na viongozi wengi wengine. Mali zao zimetaifishwa, vita dhidi ya ufisadi sio rahisi, lakini hamna kukata tamaa.

Japo jambo nzuri kwetu ni kwamba katiba ndio inafanya kazi, hivyo wote wanaofutwa kazi na kukamatwa na kwa mujibu wa katiba, sio kama huko kwenu rais anaamka kila siku akiwaza wapi pa kushtukiza. Kila kitu kipo kwenye mikono ya mtu mmoja.
 
Huku kwetu kuna chombo maalumu kinaitwa TAKUKURU na sio Rais anashughulika na Ufisadi, na mpaka sasa mkuu wa mamlaka ya mapato Taifa yuko rumande na wabunge wengine watatu.
Pamoja na hayo wengine 18 kesho ama kesho kutwa wanafuatiliwa kusweka rumande tena.


Huko kwenu wanatiwa ndani wasio wakikuyu, wakikuyu wanapeta tu, ukijuana na Rais unapeta.

Ngoja nikuwekee link za Daily Nation hapa za wala rushwa wakubwa Kenya wanaopeta mtaani mnaishia kukamata vimtu vidogo vidogo.

Njooni Tanzania tuwafundishe namna ya kuongoza nchi
 

Ndio maana nikasema unakariri taarifa za vijiweni na kuamini kuwa kweli.
Hapa kuna mawaziri wawili Wakikuyu wamefutwa kwa ufisadi na mmoja tayari yuko mahakamani wakati mwengine anafanyiwa uchunguzi.

Kwenu huko mnashtukiza watu wadogo wadogo. Hivi yule waziri Makamba sakata yake iliisha vipi ama ndio hivyo kuna wale wasioguzwa.
 
Sasa nimeamini maneno ya Godbless Lemma,mbunge wa ARUSHA,yale mashaka yake juu ya matumizi na kipato cha Zitto Kabwe kipindi hicho akiwa bado mbunge na mwanachama wa CHADEMA na mwenyekiti wa PAC,hivi yeye na Filikunjombe haya madudu ya NSSF hawakuyaona au ndio ulikuwa mradi wao?!
 
Sakata la Instagram??
Lililoanzishwa na mwanamke anayejiuza huko Marekani??

Labda serikali ya Kenya ndio inaweza kushugulikia hizo ishu
 
Kunanchi watuwake wanapiga pesa ndani ya E.A kama Kenya!!
hiyo nipesa !! Nikianza kuweka kiwango cha ufisadi kenya mbona nihatari na bado kenyatta anachekelea
 
Nadhani NSSF ndio baba lao... Yani unasoma mpaka unafikicha macho pengine macho yanasoma vibaya! Pheeeeeeww..
 
Jamaa atakuwa amebaki mkiwa sana wale wapambe wake yule mmoja wanamuita meya wa london watakuwa wamemkimbia wakati walikuwa wanashinda nae ofisini
 
Zitto Kabwe na PAC yake kweli hawakuyaona haya?Au ndiyo sababu ya Zitto kufikia kudharau hadi kuchukua posho halali Bungeni

Corrupt kid!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…