NSSF na fao la kujitoa

Wakuu hizi fedha zinatumika ktk matumizi mengine ndugu. ndio maana mafao yako ya hovyo sana na hayana tija kwa mstaafu
 
Niliachishwa kazi Ila ni miezi kadhaa sasa sijapata ela yangu kutoka mfuko na fomu nilijaza mda sana .Je nichukue hatua gani? Mana nimechoka kufuatilia au nipate direct contact ya muheshimiwa ndo watanipa.
 

Naona kila mwana CCM analikwepa suala la FAO LA kujitoa kama vile ni Jambo dogo. Bwana Humprey Polepole ameongea na waandishi wa habari Mara 2..hii hoja ameiruka.

Mtu amefukuzwa kazi au mkataba umeisha, NSSF (Fao la kukosa Ajira) wanasema ulipwe 33.3 % ya Mshahara kwa miezi 6...baada ya hapo kaa miezi 18 ...ndio ulipwe.

Sheria mpya ya 2018, Raisi Magufuli alisaini, lakini baadae akaja kufuta kikokotoo cha wastaafu pekee...Sasa wafanyakazi wanaofukuzwa kazi sekta binafsi kabla ya umri wa kustaafu wanataabika. Wenye kuona hili wamshauri Magufuli haraka sana na arekebishe maana Katiba imempa mamlaka.

Raisi Magufuli, rudisha FAO LA kujitoaa. watu walipwe pesa zao kwa mkupuo bila masharti ... Hiki ni kipindi cha Kampeni...Kura za Wafanyakazi sekta binafsi ni mamilioni...

Ndugu Bashiru na Pole pole...FAO LA Kujitoa..
 
Habari wakuu

Naomba msaada mwenye kujua kama fao la kujitoa nssf lipo au ndo mpaka unitimize miaka 55....

Mtaani kugumu kama lipo tukachukue hizo hela tufanye hata biashara.
Halipo na 55yrs hujitoi, bali unastaafu.
 
Rais hajafuta kikokotoo kipya, bali amesitisha kisitumike mpaka mwezi wa tatu mwakani.
 
Kanuni za fao la kukosa ajira..Hakuna kulipwa kwa mkupuo.

Yanalipwa 33.3 ya mshahara kwa miezi 6
 
Rais Rudisha FAO la kujitoa....

Hii kanuni ya NSSF ya 33% mshahara haifai hata kdg...

Ada na Kodi ya Nyumba mtu analipa kwa 33%?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…