NSSF inatutesa tuliopoteza ajira

NSSF inatutesa tuliopoteza ajira

Bozi

Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
92
Reaction score
144
Hali ni tete kwa tuliopoteza ajira, maisha ni magumu familia zetu zinateseka sana. Kapesa kadogo kalikokuwa kanaenda NSSF kwa miaka na miaka nako huwezi kupewa. unatakiwa mpaka ufikishe umri wa miaka 60, ni mlima mrefu huo ukiwa huna kazi.

Wanakuambia watakuwa wanakulipa 33% ya uliokuwa mshahara wako kwa miezi sita, na hilo utasugua miguu ofisi za NSSF mpaka uchakae, hakuna hela. Ni kama vile ni fao hewa.

Hivi kuna nini kimetokea katika shirika hili? hakuna mtu anapenda kupoteza kazi aje kudai hizo hela, kazi katika private sector zinapotea ghafla na bila kutegemea kipindi hiki. Tanzania kwa sasa ajira mpya ni chache sana, ati ukipoteza kazi leo, kesho utapata nyingine.
Inasikitisha na kuumiza nafsi unapoona watoto wako wanarudishwa shule kwasababu umeshindwa kulipa ada, huwezi kumudu hata gharama za matibabu, wakati unapesa mahali. Inamaana gani ktk umri wa miaka 60, upewe pesa, wakati watoto walishakosa shule?

Nikiwa bado na umri wa miaka hii 46, pesa yangu inamaana zaidi kwani naweza kuitumia kuwekeza na ikafaa kwa familia yangu kuliko sasa kubakia huko na mie maisha yangu kubomoka.

Sasa tunaanza kuuza hata thamani tulizozikusanya ilikujikimu, tuoneane huruma basi, mambo ya kusubiri mpaka umri wa miaka 60 libakie kwa watumishi wa umma ambao kazi zao ni za kudumu hata dahali.
 
Mi naona kma end of contract ela unapewa ila ndio inaprocess sana
 
Mi nilianza kazi na miaka 24 nilipofikisha miaka 29 kampuni ikaanza kupigwa dhoruba(makinikia) mikataba hawatoi nikaresign nijifanye mjasiriamali wakaniambia nisubirie mpk miaka 60. Napambana na hali yangu...karibu kijiweni mkuu bora wewe bado miaka 14, mie mpk sasa imebaki miaka 25 nasubiria mil8 ntalipwa mwaka 2044
 
Kuna utofauti kati ya kuresign n end contact hpa moja anastairi kupewa ela yke
 
dojonase mkataba gani unaoongelea? Kuacha kazi ni kuacha tu na unakua umekoma kuchangia mfuko wa jamii. Mi nilikua na mkataba miaka 3,halaf mi2 baadae wanatoa kwa miez 6/3 na yote nimechangia
 
Mi nilianza kazi na miaka 24 nilipofikisha miaka 29 kampuni ikaanza kupigwa dhoruba(makinikia) mikataba hawatoi nikaresign nijifanye mjasiriamali wakaniambia nisubirie mpk miaka 60. Napambana na hali yangu...karibu kijiweni mkuu bora wewe bado miaka 14, mie mpk sasa imebaki miaka 25 nasubiria mil8 ntalipwa mwaka 2044
Zimeshaliwa hizo.
 
Mbona hela zinatoka.
Mimi yangu nimechukua kabla ya pasaka, na iliwekwa yote na nimetafuna yote kwenye mambo yafaayo.
Ila hata nlipokuwa naisotea miezi nane sikutetereka maana nlishaseti mipango ya kuniingizia chochote. Fuatilia tu mkuu utaipata.
 
Pole sana ndugu, rais sialisema watu walipwe pesazao kama kawaida hadi 2023?.

Nini kimetokea tena, wanakaidi maelekezo,?.

Kwa private sector ni uonevu kumuambia mtuasubiri mbaka afikishe miaka 60.
 
Hali ni tete kwa tuliopoteza ajira, maisha ni magumu familia zetu zinateseka sana. Kapesa kadogo kalikokuwa kanaenda NSSF kwa miaka na miaka nako huwezi kupewa. unatakiwa mpaka ufikishe umri wa miaka 60, ni mlima mrefu huo ukiwa huna kazi.

Wanakuambia watakuwa wanakulipa 33% ya uliokuwa mshahara wako kwa miezi sita, na hilo utasugua miguu ofisi za NSSF mpaka uchakae, hakuna hela. Ni kama vile ni fao hewa.

Hivi kuna nini kimetokea katika shirika hili? hakuna mtu anapenda kupoteza kazi aje kudai hizo hela, kazi katika private sector zinapotea ghafla na bila kutegemea kipindi hiki. Tanzania kwa sasa ajira mpya ni chache sana, ati ukipoteza kazi leo, kesho utapata nyingine.
Inasikitisha na kuumiza nafsi unapoona watoto wako wanarudishwa shule kwasababu umeshindwa kulipa ada, huwezi kumudu hata gharama za matibabu, wakati unapesa mahali. Inamaana gani ktk umri wa miaka 60, upewe pesa, wakati watoto walishakosa shule?

Nikiwa bado na umri wa miaka hii 46, pesa yangu inamaana zaidi kwani naweza kuitumia kuwekeza na ikafaa kwa familia yangu kuliko sasa kubakia huko na mie maisha yangu kubomoka.

Sasa tunaanza kuuza hata thamani tulizozikusanya ilikujikimu, tuoneane huruma basi, mambo ya kusubiri mpaka umri wa miaka 60 libakie kwa watumishi wa umma ambao kazi zao ni za kudumu hata dahali.
Safi sana labda ndio mtajifunza.
 
Ile ilikuwa zuga mkuu, utafuatilia pesa zako mpk soli za viatu vitakwisha na fedhwa zako hupati.. Mfano me ni muhanga wa hilo. Ukifika wanakuambia subiri miaka 55 yaani mtu yeyote anayeshabiki CCM/serikali yake nawaona ni mashetani.vijana tunasumbuka mitaani wao wamekalisha matako yao bungeni kupitisha sheria za ki.s..nge
Pole sana ndugu, rais sialisema watu walipwe pesazao kama kawaida hadi 2023?.

Nini kimetokea tena, wanakaidi maelekezo,?.

Kwa private sector ni uonevu kumuambia mtuasubiri mbaka afikishe miaka 60.
 
Sina zaidi ya kusema poleee nakuomba tafadhali usijichanganye kwenye vilabu utapoteza mwelekeo
 
Pole mkuu, Serikali iliyoshindwa kuongoza huanza kugombana na raia wake.
 
Back
Top Bottom