NSSF ichunguzwe matumizi mabaya ya hela za wafanyakazi

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
Kuna mambo mengi hayaeleweki uamuzi unatolewaje kutumia fedha zetu sisi wavuja jasho ambazo zimehifadhiwa na NSSF na mashirika mengine kama hayo, bila kujua zitarudi vipi:

1. Hivi karibuni NSSF ilitoa msaada kwa watu walioathirika na mafuriko, hizi sio hela zao, wamepewa wawatunzie wafanyakazi, sasa wao wanaanza kuzitafuna na kutoa misaada, mwisho wa siku wanashindwa hata kuweka inflation rate katika hela za wastaafu

2. Kuna hizi hela zilizoliwa na NIP wakati jengu husika lipo vilevile: Kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya mwaka 2012/13, imebaini kiasi cha dola za kimarekani 1,532,458.91 zilizotolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) zimetumika kinyume na taratibu za kisheria.

Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Profesa Samweli Wangwe, Mwenyekiti wa NIP, amesema kuwa, fedha hizo zilikua za mkopo kwa ajili ya uendelezaji wa jengo la Maarifa lililopo mtaa wa Ohio na Hollis jijini Dar es Salaam ambalo linamilikiwa na Shirika hilo zilipo.

Amesema, ripoti hiyo ilionyesha kuwa, kiasi cha dola za kimarekani 480,000 zilitumika kuilipa kampuni ya Zawadi Communication Limited ambayo inamilikiwa na Jamal Malinzi ambaye ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), kama gharama za udalali wa kuitafutia NIP mbia wa ujenzi wa jengo hilo ambao ni NSSF.

3. Wafanyakazi wanahangaika kukusanya hela zao ili ziwe nyingi na faida juu hapo baadae; ni muhimu bodi ya NSSF iundwe upya ishirikishe wafanyakazi wenyewe kama members wa bodi washiriki katika maamuzi ya investment na miradi mingine

4. NSSF za nchi zilizoendelea mfanyakazi anapewa mpaka hisa mbalimbali katika majengo na mali za NSSF, serikali iangalie hilo ili wafanyakazi tunufaike na hela zetu badala ya watu wachace kunuendelea kunufaika na fadha za wavuja jasho.

Mh Raisi, wewe kama kimbilio letu wananch tafadhali liangalie hili shirika kwa macho ya karibu sana
 
Back
Top Bottom