Kulingana na taarifa ya CAG, sehemu kubwa ya fedha za wanachama ambazo hazijarejeshwa, zilikopeshwa kwa serikali kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Katika chuo hiki, NSSF peke yake iliingiza Sh. 234.1 bilioni. Mifuko iliyosalia ilitoa jumla ya Sh. 181.3 bilioni.
Katika ujenzi wa UDOM, PPF ilitoa Sh. 39.99 bilioni, PSPF (Sh. 105.9 bilioni), LAPF (Sh. 22 bilioni) na NHIF (Sh. 13.4 bilioni). Fedha hizo na riba yake hazijarejeshwa.
Ripoti ya CAG, Ludovick Utouh, inasema kutorejeshwa kwa mikopo hiyo, iliyochukuliwa au kudhaminiwa na serikali, ni kinyume cha sheria ya udhamini ya mwaka 1974.
Kutolipika kwa mikopo hii iliyodhaminiwa na serikali kunaiweka mifuko hii ya hifadhi katika hatari ya kupoteza fedha za wanachama na kuhatarisha uwezo wa mifuko kufanya uwekezaji zaidi, anasema na kuongeza: