North Korea yaiduwaza dunia kwa technolojia kali.

North Korea yaiduwaza dunia kwa technolojia kali.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,330
Reaction score
17,582
_98994816_ac1fc16b-56bf-4cbb-a8ce-2225f32c2e4f.jpg

Marekani imeyataka mataifa yote kukatiza uhusiano wa kidiplomasia na ule wa kibiashara na Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanyia jaribio la kombora lake la masafa marefu.

Akizungumza katika baraza la usalama la umoja wa kimataifa ,mjumbe wa Marekani katika baraza hilo Nikki Haley amesema kuwa rais Trump amemtaka mwenzake wa China kukata usambazaji wa mafuta kwa Pyongyang.

Amesema kuwa Marekani haitaki mzozo lakini Korea Kaskazini itaangamizwa iwapo vita vitazuka.

Onyo hilo linajiri baada ya Pyonyang kufanyia majaribio kombora lake la kwanza katika kipindi cha miezi miwili.

Korea Kaskazini imesema kuwa kombora hilo lililorushwa siku ya Jumatano ambalo inasema liliruka kimo cha kilomita 4,475, ikiwa ni mara kumi zaidi ya kimo cha kituo cha angani.

Madai hayo hayakuthibitishwa na wataalam wametiliashaka uwezo wa taifa hilo kuwa na teknolojia kama hiyo.

Hatahivyo kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema kuwa uzinduzi wa kombora hilo ulikuwa wa kufana.

Jaribio hilo likiwa mojawapo ya majaribio yaliofanywa na taifa hilo limeshutumiwa na jamii ya kimataifa na tayari baraza la usalama la umoja wa kimataifa limeitisha kikao cha dharura.

Bi Haley alionya kuwa kuendelea kwa uchokozi kunalenga kuliyumbisha eneo hilo.

''Tunahitaji China kuchukua hatua zaidi'', alisema.

Rais Trump alimpigia simu rais Xi Jinping mapema siku ya Jumatano , Ikulu ya Whitehouse ilisema kuwa rais Trump alizungumza na Xi Jinping kwa simu akimtaka kuchukua hatua zozote kuishawishi Korea Kaskazini kusitisha uchokozi na kusitisha mpango wake wa kinyuklia. BBC

25f21f9a276e4a069bbca0de204c7f98_6.jpg
 
Haya mambo siyo ya kushabikia kabisa kama wengi wenu mnavyofanya humu. Ni ujinga na uwezo mdogo wa kufikiri ndio unawafanya wengi kuleta ushabiki.
Wewe lima mpunga huko uuze mchele acha wanaume watifuane wewe huhusiki
 
Aisee Third world war is coming cdhan kama watu wanaona hichi kitu coz hats first world war it was Like this aisee ngja tutaona real alliances soon
 
Kama ipo ipo tu watadundana na mwisho mbabe atajulikana, ama hii vita yaweza kumark mwisho ya dunia, ebu fikiria kama mataifa 6 yakapigana kwa nuclear yaweza kuwa hatari kwa uhai wa viumbe vyavdunia
 
Apa suluhisho ninkupiga marufuku ya kbs uwepo wa nuclear na project zake zote maana iko siku dunia itafanywa kuwa si mahali salama tena pakuishi endapo nuclear bomb itaendelea kuexist
 
Haya mambo siyo ya kushabikia kabisa kama wengi wenu mnavyofanya humu. Ni ujinga na uwezo mdogo wa kufikiri ndio unawafanya wengi kuleta ushabiki.
Bora useme wewe mtu anaokota data kutoka kwenye magazeti ya udaku ya nchi za nje anahisi anaujua huu mzozo na ukubwa wa uwezo wa kivita kati ya hizi nchi mbili.NK anaonesha anatoa siri ya makombola yake huku U.S.A hajaonesha hata moja hii haimanishi mmarekani ana mishale mwenzie ana makombora ya masafa marefu.Ikumbwe 9 aug 1945 na 6 aug 1945 mmarekani huyu huyu aliishangaza dunia kwa makombora yake ya nuclear (eroshima n Nagasaki) mpaka kupelekea kuzima vita ya pili dunia na kuundwa kwa UN
 
Marekani wanataka kuziingiza nchi nyingine katika Insecurity zao
 
Kweli mkuu, hawa jamaa wakitifuata sisi wa dunia ya tatu hali itakuwa tete.
Because Everything is not as it seem to be
 
Bora useme wewe mtu anaokota data kutoka kwenye magazeti ya udaku ya nchi za nje anahisi anaujua huu mzozo na ukubwa wa uwezo wa kivita kati ya hizi nchi mbili.NK anaonesha anatoa siri ya makombola yake huku U.S.A hajaonesha hata moja hii haimanishi mmarekani ana mishale mwenzie ana makombora ya masafa marefu.Ikumbwe 9 aug 1945 na 6 aug 1945 mmarekani huyu huyu aliishangaza dunia kwa makombora yake ya nuclear (eroshima n Nagasaki) mpaka kupelekea kuzima vita ya pili dunia na kuundwa kwa UN
Sisi tunaojua habari za migogoro tunakifahamu anachokifanya NK kutangaza uwezo wake kijeshi. Hiyo ni mbinu sahihi ya kivita. Ndo maana hata sisi wakati mwingine tunaonyesha zana zetu na makomandoo wetu hadharani mbinu ambayo imesaidia kuepusha damu na Malawi na Rwanda. Lakini ile haikumaanisha kuwa zana zile ndio zote kabisa na makomandoo wale ndio wrote kabisa. Hata Marekani anapomwambia NK kuwa ataiteketeza ni mbinu hizohozo za kumpiga adui yako kisaikolojia
 
Urusi nae amegoma kabisa kumuwekea vikwazo NK amemwambia Trump yeye ndo mchokozi, NK hana shida na mtu na hawaoni sababu ya kumuwekea vikwazo
 
Back
Top Bottom