Nooij Aita 24 kuikabili Swaziland

Nooij Aita 24 kuikabili Swaziland

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,356
10678819_452584501547510_181821595198042511_n.jpg

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland itakayochezwa Novemba 16 mwaka huu jijini Mbabane.

Akizungumza Dar es Salaam, leo (Novemba 5 mwaka huu), Nooij alisema kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 10 mwaka huu saa 6 mchana kwenye hoteli ya Accomondia, na siku hiyo hiyo jioni kitafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana.

Novemba 11 mwaka huu, Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka kwenda Afrika Kusini ambapo itaweka kambi ya siku mbili kabla ya kuondoka Novemba 13 mwaka huu kwenda Swaziland.

Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni makipa Aishi Manula (Azam) na Deogratias Munishi (Yanga). Mabeki ni Abubakar Mtiro (Kagera Sugar), Aggrey Morris (Azam), Emmanuel Simwanda (African Lyon), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Osacr Joshua (Yanga), Said Moradi (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shomari Kapombe (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Haruna Chanongo (Simba), Himid Mao (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Said Ndemla (Simba) na Salum Abubakar (Azam).

Washambuliaji ni Juma Luizio (ZESCO, Zambia), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo).


Chanzo: TFF
 
Enzi hizo, taarifa kama hii ilivyokua ikitoka, kesho yake waandishi wetu wa sports wanakuja na heading kama,

"Azam Fc yazigaragaza vibaya Simba na Yanga, Taifa!"

Ukifunua gazeti, utakuta,

"...ni baada ya wachezaji saba wa Azam Fc kuitwa Taifa Stars, huku wachezaji sita toka Yanga wakijumuisha, Simba ikiambulia wachezaji watatu tu.."

Nazimisi sana hizi siku.
 
Abuu Mtiro?

Huyo jamaa wa kitambo sana, nakumbuka mechi moja ya kombe tusker kati ya Simba na Yanga ilipigwa CCM Kirumba alitandika shuti moja Kaseja akadaka hewa na mpira ukagonga nguzo na kutoka. Halafu baada ya muda kidogo Victor Costa akalambwa red, pamoja na Simba kucheza pungufu kwa muda wa zaidi ya dakika 70 mwisho wa mchezo Simba 2 na Yanga 0, magoli ya Emanuel Gabriel na Musa Hassan Mgosi.

Kipindi kile ilikuwa Simba ya ukweli hakuna majonzi kama sasa.
 
Noij nae bwana! sasa Mtiro na uzee wote starz anaenda kufanya nn!!! huyu kocha nae kimeo kwel...

Amesema ajaona mchezaji anayetumia mguu wa kushoto kwa sasa mwenye uwezo wa kuchezea mpira kama Abuu Mtiro kwa beki ya kushoto na ndio maana amemuita ili kumuangalia
 
Back
Top Bottom