PreGE2025 No reforms no election ni muhimu kuliko tunavyoichukulia

PreGE2025 No reforms no election ni muhimu kuliko tunavyoichukulia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Madwari Madwari

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2014
Posts
2,732
Reaction score
4,552
Anachotetea Tundu Lissu kina umuhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Uongozi ni kitu kinachofanyika kwa referal na sheria za nchi zinafanyika kwa referal. Magufuli ndiyo Rais wa kwanza Tanzania aliyetumia nguvu zake kwa asilimia 100%. Tulishuhudia alijenga Airport alikozaliwa. Alijaza watu wa kanda ya ziwa serikalini. Na hadi kupeleka Tawi la benki Chato. Ni rais wa kwanza Tanzania ambaye aliteuwa binamu yake BITEKO kuwa waziri.

Baada ya Magufuli kufariki tukampata Mama Samia. Mama wasukuma wa mama wakawa wazanzibari na chati ya Mama ndiyo Kizimkazi. Na hakuna mtu wa kumfanya Mama Samia lolote maana katiba inaruhusu. Na mama akafuata nyayo kwa kumpa Mkwe wake Mchengerwa Uwaziri.

Hivi sasa kila mtu ambaye yupo serikalini ameshajua nguvu ya Rais. Maana kabla ya Magufuli marais walikuwa na ubinadamu kidogo au ustaarabu. Kama serikali ni gari Magu alikanyaga mpaka 180 km/ h.

Umuhimu wa NO REFORM NO ELECTION ni kuamsha watu na kuweka nafasi ya nguvu ya wananchi kusikilizwa na kuweka watu sahihi serikalini. Kufanya hivi kutazuia Tanzania kuja kuwa kama Congo, maana ndiko tunakoelekea. Hatuna viongozi wastaarabu wala waoga wa kutenda maovu. Magufuli aliwaonyesha watu wote utamu wa Urais. Na kila mwanasiasa anatamani urais kwa manufaa yake mwenyewe. Ili kuvunja uongozi wa kauli ya mtu mmoja ni muhimu kuweka watu sahihi na kuipa nchi katiba mpya. Muda ndiyo huu maana tukielekea na hii katiba, tutapata Rais mithili ya Mobutu wa Zaire.

Kumfungulia Tundu Lissu kesi hakumdhooofishi bali kunamjenga na kumuongezea CV. Matendo kama haya yanadhihirisha kuwa hatuna watu makini katika TISS. CV ya Tundu lissu ni kubwa sana hakuna mwanasiasa toka uhuru aliyepigwa risasi 64 na kwa ajili ya nchi yetuya Tanzania. Hakuna mwanasiasa anaweza kuifikia hiyo CV. Kumfungulia kesi ya uhaini ni kumuongezea CV na kumpaisha zaidi Lisu. Mnataka muendeshe kesi mitandaoni mahakama haina infrastractire ya ku-stream kwa stakeholders wote. Unadhani solutioni itakuwa nini zaidi ya ku-stream kesi youtube ? Na mkipeleka kesi youtube ni faida au hasara kwa Lisuu ? Kwa sasa hakuna njia pekee bali maelewano. Kama mgetaka kukipasua chama cha CHADEMA mngesubiri kwanza wasign kanuni za maadili ndiyo mumkamate Lissu. Sasa kuonyesha ujinga wa TISS mnamkamata lissu wakati kanuni hazijasainiwa. Utakipasuaje chama wakati hata kama wale G55 kwa sasa hawana pointi maana chama hakina sifa ya kushiriki uchaguzi kisheria. Aisee usalama wetu wa taifa unafanya kazi gani ? Yaani hawawezi ku-foresight na ku- forecast mambo madogo kama haya.
 
Wasichokifahamu watawala ni kitu kimoja tu! No reform no election inaungwa mkono na wananchi wote wapenda mabadiliko (pasipo kujali tofauti zao za kiitikadi), na pia waliochoshwa na huu mfumo wa utawala wa sasa uliojaa hila, vitisho, ubaguzi, upendeleo, rushwa, ufisadi, unyanyasaji, utekaji, na kila aina ya uovu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom