PreGE2025 No reform, no election ni kukimbia kushindana!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
5,414
Reaction score
15,456
Kumekuwa na kauli inayozidi kushika kasi miongoni mwa wanasiasa wa upinzani: “No reform, no election.” Wana maana gani? Wanataka kusema kuwa hawatashiriki uchaguzi mpaka marekebisho ya mfumo wa uchaguzi yafanyike. Lakini je, hii ni hoja ya msingi au kisingizio cha kukwepa ushindani?

1. Marekebisho si kisingizio cha kukwepa uchaguzi

Kila mfumo wa uchaguzi duniani una mapungufu, hata nchi zilizoendelea bado zinakumbana na changamoto mbalimbali za uchaguzi. Lakini wanasiasa wa kweli hawawezi kusubiri mfumo uwe “mkamilifu” ndipo washiriki. Wanaingia kwenye uchaguzi, wanapambana na kushinda kwa hoja.

2. Historia inaonyesha wapinzani wameshinda hata bila marekebisho makubwa

Katika chaguzi zilizopita, wapo wagombea wa upinzani walioshinda nafasi mbalimbali, kutoka madiwani hadi wabunge. Kama mfumo ni mbovu kiasi hicho, waliwezaje kushinda? Tatizo ni hoja dhaifu na maandalizi mabaya, si mfumo wa uchaguzi pekee!

3. Kushiriki ni njia bora ya kushinikiza mabadiliko

Mabadiliko makubwa ya mfumo wa uchaguzi hayawezi kupatikana kwa kususa. Kushiriki uchaguzi ni fursa ya kupata wawakilishi wa kusukuma mabadiliko ndani ya mifumo rasmi, kama bungeni. Wanasiasa wanaokaa nje ya uwanja wakilalamika hawawezi kuleta mabadiliko yoyote.

4. Wananchi wanahitaji viongozi, si maneno matupu

Mtu anaposema “No reform, no election” anamaanisha nini kwa wananchi? Anawaambia wasiwe na viongozi wa kuwawakilisha? Siasa ni mapambano, na anayekataa kuingia ulingoni hana nia ya kweli ya kuwatumikia wananchi.

Badala ya kauli ya “No reform, no election,” tunahitaji kauli ya “Tunaingia na tunashinda.” Mabadiliko hayaletwi kwa maneno, bali kwa vitendo. Wanasiasa wanaoamini katika mabadiliko ya kweli wanapaswa kupambana ndani ya mfumo uliopo huku wakisukuma mabadiliko wanayoyataka.
 
Huna akili mleta mada.

Umaongelea upinzani kushinda chaguzi zilizopita unadhani walishinda kirahisi?

Hujui Kamanda wa Polisi Wankyo alimwambia msimamizi wa uchaguzi asipotangaza matokeo yaliyompa ushindi Lissu angetoa polisi wanaolinda ndo ilibidi Lissu atangazwe kuwa mbunge?

Hujaona engua ya wagombea wa upinzani mwaka 2019, 2020 na juzi 2024?

Acha kujidharirisha humu ndani. Hata kama mnalipwa kufanya spinning sio ndo mjitoe ufahamu kwa kiwango hicho.
 
Acha ujinga wewe, uchaguzi gani wa kijinga unashauri watu washiriki yaani hadi watu wafe ndio mtu atangazwe. Mwanza pale mwaka 2010 watu walivamia ofisi za jiji na kutaka kuzichoma moto ndio kamanda Sirro akiwa RPC akamwambia mkurugenzi atangaze matokeo hiyo ni baada ya siku 3
 
Kwahiyo watu waendelee kushiriki kama wajinga huku wakiuliwa na kuachwa na vilema vya maisha. Hakuna anayeogopa ushindani, ila chaguzi zetu kwa sasa sio ushindani tena, bali ni kuhalakisha ccm kukaa madarakani kwa damu za wapinzani.
 
Kumekuwa na kauli inayozidi kushika kasi miongoni mwa wanasiasa wa upinzani: “No reform, no election.” Wana maana gani? Wanataka kusema kuwa hawatashiriki uchaguzi mpaka marekebisho ya mfumo wa uchaguzi yafanyike. Lakini je, hii ni hoja ya msingi au kisingizio cha kukwepa ushindani?

1. Marekebisho si kisingizio cha kukwepa uchaguzi

Kila mfumo wa uchaguzi duniani una mapungufu, hata nchi zilizoendelea bado zinakumbana na changamoto mbalimbali za uchaguzi. Lakini wanasiasa wa kweli hawawezi kusubiri mfumo uwe “mkamilifu” ndipo washiriki. Wanaingia kwenye uchaguzi, wanapambana na kushinda kwa hoja.

2. Historia inaonyesha wapinzani wameshinda hata bila marekebisho makubwa

Katika chaguzi zilizopita, wapo wagombea wa upinzani walioshinda nafasi mbalimbali, kutoka madiwani hadi wabunge. Kama mfumo ni mbovu kiasi hicho, waliwezaje kushinda? Tatizo ni hoja dhaifu na maandalizi mabaya, si mfumo wa uchaguzi pekee!

3. Kushiriki ni njia bora ya kushinikiza mabadiliko

Mabadiliko makubwa ya mfumo wa uchaguzi hayawezi kupatikana kwa kususa. Kushiriki uchaguzi ni fursa ya kupata wawakilishi wa kusukuma mabadiliko ndani ya mifumo rasmi, kama bungeni. Wanasiasa wanaokaa nje ya uwanja wakilalamika hawawezi kuleta mabadiliko yoyote.

4. Wananchi wanahitaji viongozi, si maneno matupu

Mtu anaposema “No reform, no election” anamaanisha nini kwa wananchi? Anawaambia wasiwe na viongozi wa kuwawakilisha? Siasa ni mapambano, na anayekataa kuingia ulingoni hana nia ya kweli ya kuwatumikia wananchi.

Badala ya kauli ya “No reform, no election,” tunahitaji kauli ya “Tunaingia na tunashinda.” Mabadiliko hayaletwi kwa maneno, bali kwa vitendo. Wanasiasa wanaoamini katika mabadiliko ya kweli wanapaswa kupambana ndani ya mfumo uliopo huku wakisukuma mabadiliko wanayoyataka.
Magugu huota kirahisi kuliko mazao, upumbavu na ujinga ni rahisi sana kuupata kuliko werevu.
 
Unashindana ushinde wakati umefungwa mikono mbele ya adui aliye HURU,mkuu upo sawa kweli kichwani?
Au ndio wale wale mlioshiba hela za Abdul kama akina Wenje na Mrema?
 
Swali rahisi iweje likutoe kamasi wakati wa kulijibu
 
Kumekuwa na kauli inayozidi kushika kasi miongoni mwa wanasiasa wa upinzani: “No reform, no election.” Wana maana gani? Wanataka kusema kuwa hawatashiriki uchaguzi mpaka marekebisho ya mfumo wa uchaguzi yafanyike. Lakini je, hii ni hoja ya msingi au kisingizio cha kukwepa ushindani?

1. Marekebisho si kisingizio cha kukwepa uchaguzi

Kila mfumo wa uchaguzi duniani una mapungufu, hata nchi zilizoendelea bado zinakumbana na changamoto mbalimbali za uchaguzi. Lakini wanasiasa wa kweli hawawezi kusubiri mfumo uwe “mkamilifu” ndipo washiriki. Wanaingia kwenye uchaguzi, wanapambana na kushinda kwa hoja.

2. Historia inaonyesha wapinzani wameshinda hata bila marekebisho makubwa

Katika chaguzi zilizopita, wapo wagombea wa upinzani walioshinda nafasi mbalimbali, kutoka madiwani hadi wabunge. Kama mfumo ni mbovu kiasi hicho, waliwezaje kushinda? Tatizo ni hoja dhaifu na maandalizi mabaya, si mfumo wa uchaguzi pekee!

3. Kushiriki ni njia bora ya kushinikiza mabadiliko

Mabadiliko makubwa ya mfumo wa uchaguzi hayawezi kupatikana kwa kususa. Kushiriki uchaguzi ni fursa ya kupata wawakilishi wa kusukuma mabadiliko ndani ya mifumo rasmi, kama bungeni. Wanasiasa wanaokaa nje ya uwanja wakilalamika hawawezi kuleta mabadiliko yoyote.

4. Wananchi wanahitaji viongozi, si maneno matupu

Mtu anaposema “No reform, no election” anamaanisha nini kwa wananchi? Anawaambia wasiwe na viongozi wa kuwawakilisha? Siasa ni mapambano, na anayekataa kuingia ulingoni hana nia ya kweli ya kuwatumikia wananchi.

Badala ya kauli ya “No reform, no election,” tunahitaji kauli ya “Tunaingia na tunashinda.” Mabadiliko hayaletwi kwa maneno, bali kwa vitendo. Wanasiasa wanaoamini katika mabadiliko ya kweli wanapaswa kupambana ndani ya mfumo uliopo huku wakisukuma mabadiliko wanayoyataka.
Kitu unachoongea ni hopeless kabisa ,usichukulie mifano ya uchaguzi wa nyuma na uchaguzi kuanzia 2019 mpaka 2024 hizo zama ni mbingu na Ardhi hazifanani hata kidogo.kipindi cha nyuma wagombea walikuwa hawaenguliwe hivi sasa robo tatu ya wagombea wanaenguliwa.Vituoni kura zilikuwa zinapigwa vizuri na kuhesabiwa na kila wakala anapata idadi ya kura za mtu wake aliye msimamia hivi sasa huo utaratibu hakuna,ilikuwa kura zikimaliza kuhesabiwa katka kituo idadi ya kura za kituo hicho kuanzia ,diwani,mbunge na raisi ,, zinabandikwa nje yakituo siku hizi hilo halipo,Zamani wasimamizi wauchaguzi hawakuwa makada wa chama chochote,hivi sasa mpaka wakurugenzi na makamishina wa tume ni makada.Zamani kampeni zilikuwa huru na hazikuwa zinaingiliwa kwa kiasi kikubwa na vyombo vya dola.Hivi sasa vyombo vya dola vinataka wewe uzungumze yale yatakayo wafurahisha wao ,badala yakumuachia msajili havichukulie hatua vyoma vinavyokwenda kinyume na usajili vyombo vya dola ndivyo vinajifanya wao ndiyo regulator wa siasa.kwahiyo msajili yeye anabaki kama kibogoyo.Ushindani kwa sasa hauwezekani kwakuwa mfumo wa uchaguzi uehabiwa makusudi.Pia sheria nyingi pia zimevurugwa makusudi,tofauti na zamani,uchaguzi huru na haki hauwwzekani tena Tanzania ,pamoja na hao CDM kusema no reform no ele,,ection lakini asilimia kubwa watu hawajitokezi kwenye chaguzi ,idadi za matokeo huwa hazina uhalisia na wapiga kura ndiyo maana huwa hawataki kubbandika matokeo na kutoa nakala za matokeo kwa mawakala.Serikali isipo rekebisha hii hali viongozi watakao patikana watakuwa ni viongozi wasiyo na ridhaa ya wananchi. Na viongozi wanamna hiyo hawawezi kuwaletea maendeleo wananchi kwa sababu hawakuwekwa pale kwa matakwa ya wananchi.Serikali ya CCM bado inauwezo wakuliangalia hilo na kulirekebisha.Lakini wakijiona kuwa wao ni wanufaika wa mfumo uliopo sasa watadidimiza nchi nakusababisha uchumi wa nchi kuangamia kabisa.Bado nafasi ipo.Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom