Kule sina uhakika sana maana yule dogo naye hakuwa malaika.
Kwa sababu kabla ya encounter yake na polisi alikuwa keshatoka kupora duka.
Hii ya Eric Garner na yule dogo ni ishu mbili tofauti.
Eric Garner hata hakutishia maisha ya mtu yoyote na karibu kila kitu kiko on tape.
Mtu anayeuza visigara (hata kama ni kinyume na sheria) na mtu aliyetoka kupora duka la mtu akasimamishwa na polisi halafu akaleta ukaidi uliopelekea kutokea mtafarufu, sidhani kama vinalingana.
Labda kama kuna mlinganyo basi ni ule wa wote wawili kupoteza maisha yao ingawa ni katika mazingira tofauti kabisa.
Na nina imani kuwa watu wengi, weupe kwa weusi wana sympathy kwa kilichomtokea bwana Garner kuliko huyo Mike Brown.
kaka nakuelewa ila mimi naijua bunduki,huwezi ku_fire kwa raia ambaye hajatishia uhai wako au wa wengine,na km mwizi hana silaha basi mpge risasi ya mguu,madogo wamepnda sana lakn kutoa uhai ni kesi nyingne,uhai hauna matibabu,sio mali kuwa itatafutwa tena