Habari mkuu, kwanza napenda kukujuza kuwa, kwenye uombaji mikopo mara nyingi wanaangalia shughuli unayoifanya ambayo ndio inayokuingizia kipato (uwe umeajiriwa ama umejiajiri), na kiasi unachoweza kupewa kinategemea na dhumuni la mkopo, kipato chako, historia yako ya ukopaji, kumbukumbu zako na dhamana zako. Ila si kwamba ukiwa na dhamana yenye thamani kubwa peke yake ndio kwamba utaweza kupata mkopo. Na masharti nafuu ya mikopo ni pamoja na riba ndogo, muda wezeshi kwa mteja kuweza kulipa, uhakika na uharaka wa huduma bora za utoaji mikopo. Hivyo nakushauri upitie Bank na taasisi mbalimbali za mikopo kuangalia vitu hivyo ili uweze kujua ipi ni nafuu kwako.
Recommended: FINCA, Advans Bank, Akiba Commercial Bank.