Naomba kuuliza bank ipi ni rafiki kwa mikopo yenye riba rafiki na hakuna longolongo kwenye kutoa mkopo??

mriringa

JF-Expert Member
Jan 17, 2017
316
500
Nina wiki mbili tangu niombe mkopo bank ya CRDB lakini hadi sasa sijaingiziwa pesa. Jana nimeenda kufuatilia nikakutana na watu kibao nao wanalalamika tena mwingine aliomba mkopo wa kumuuguza mamake lakini hadi mamake kafariki bila kupata mkopo na ni miezi 2 toka aombe.

Nilitafakari sana juu ya kifo za mama huyo maana huenda kafa kisa kakosa matibabu ambayo mwanae alijitoa kumhudumia ila CRDB bank wakazingua. Nawaza nijitoe na namna ya kujitoa nataka nichukue mkopo bank nyingine na mshahara ubakie 2/3 pekee ambayo haiwezi kukatwa kwa vyovyote.

Note nachukua mkopo kwaajiri ya matibabu ya babangu ambae anatakiwa kufanyia huduma ya figo iliyofeli.

Kama kuna anayejua bank yenye riba nafuu na mkopo unatoka haraka anisaidie.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom